Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango amepokea vifaa tiba kwa ajili ya Watoto Njiti kutoka Taasisi ya Doris Mollel na vifaa tiba kutoka Tume ya Taifa ya Ushindani katika Hospitali ya Wilaya ya Buhigwe, Kigoma Julai 06, 2023.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango amefungua Hoteli ya Kisasa ya Bwami Dubai iliopo Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma Julai 05, 2023.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango amepokea Madarasa, Samani mbalimbali na Ofisi za Walimu yaliokarabatiwa na Benki ya Biashara Tanzania (TCB) katika Shule ya Msingi Muyama wilayani Buhigwe, Kigoma Julai 05, 2023.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango amezindua Tawi la Benki ya NMB Wilaya Buhigwe mkoani Kigoma Julai 04, 2023.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo amefanya mazungumzo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hamza Hassan Juma Jijini Dodoma Julai 4, 2023.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga akutana na Watendaji waandamizi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Faru Graphite Corporation jijini Dodoma Juni 27, 2023.