Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Historia ya Ofisi ya Makamu wa Rais

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa tarehe 26 Aprili, 1964. Baada ya Muungano, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheikh Abeid Karume akawa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Rashidi Mfaume Kawawa alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Tanzania na kiongozi wa shughuli za Serikali katika Bunge.

Mwaka 1992, Tanzania ilipitisha Mfumo wa Demokrasia ya Vyama vingi ambao ulihitaji marekebisho makubwa ya Katiba. Marekebisho haya yalihusu suala la Makamu wa Rais na kuanzishwa mfumo wa mgombea mwenza uliowaunganisha mgombea Urais na Makamu wa Rais. Hii ilimaanisha kwamba, Rais wa Zanzibar aliacha kuwa Makamu wa Rais wa Muungano moja kwa moja lakini akawa Mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Muungano.

Settings