Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Mhandisi Masauni aridhishwa utunzaji mazingira Geita

Mar, 15 2026

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni aipongeza Shule ya Sekondari ya Wasichana Geita pamoja na Mgodi wa Dhahabu wa Geita( Geita Gold Mines) kwa kutunza Mazingira, kurejesha mazingira katika hali yake ya awali baada ya kumaliza uchumbaji pamoja kuhakikisha kuwa asilimia kubwa ya ajira inakwenda kwa Watanzania.

Mhe Masauni ameyasema hayo baada ya kutembelea shule hiyo ya Wasichana iliyopo kata ya Bomba Mbili Mkoani Geita Machi 14,2026, huku akiwa ameambatana na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi, Mkurugenzi Mkuu NEMC na Wataalam kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na NEMC.

Akizungumza jinsi shule hiyo ilivyoitikia agizo la matumizi ya Nishati safi ya kupikia Mwalimu ‘Mkuu wa Shule hiyo Bi. Mwamini George Kagoma, ameeleza kuwa shule hiyo ilianza matumizi ya Nishati safi ya kupikia kuanzia mwaka 2025 ambapo matumizi ya nishati hiyo yameleta manufaa mbalimbali ikiwa pamoja na kupunguza gharama ya ununuzi wa Kuni na Mkaa, kuokoa muda, kulinda afya kwa kupunguza hewa chafu na chakula kuiva kwa wakati na mazingira ya jiko kuwa safi.

Mwalimu Mwamini ameeleza kuwa shule hiyo imetumia kiasi cha Tsh 24,105,080/- kufunga Mfumo wa Nishati safi ya kupikia, ikiwa ni gharama ya awali ya mapato ya ndani, aidha shule imekua ikitumia wastani wa Kilo 1,000 za gesi ya kupikia yenye thamani ya Tsh 3,000,000/- sawa na wastani wa Tsh. 54,700/- kwa siku kiasi ambacha kama ingekuwa ni kuni au Mkaa usingetosha kupika milo mitatu ya wanafunzi 525 na Waalimu 25 kwa siku.

Akizungumza kuhusu suala la utunzaji wa Mazingira Meneja wa Mazingira GGM Bw. Yusuph Mhando, amesema Geita Gold Mine ina sera ya usimamizi wa Mazingira ambayo inazingatua matakwa ya sheria ya viwango vya kimataifa, GGM inahakikisha kuwa Utunzaji wa Mazingira ikiwa ni pamoja na ubora wa hewa, udhibiti wa vumbi na gesi ni vya kisheria.

Ubora wa maji, Sauti, Mitetemo ya Vilipuzi jamii wanaelishwa kuhusu athari zake. Aidha katika kutambua fursa mbalimbali za Taka Mgodi wa Geita, unatenganisha taka na kuzilejeleza.

Habari

Settings