Habari
Dkt Muyungi ateta na GCF
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Uwekezaji Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi (GCF) Dkt. Achala Abeysinghe Juni 16, 2026 jijini Bonn, Ujerumani.
Kikao hicho cha pande mbili baina ya Jamhuri ya Muungano waTanzania na GCF kimfanyika kando ya Mkutano wa 64 wa Kamati za Utekelezaji na Sayansi na Ushauri chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (SB64) ukiendelea.
Madhumuni ya kikao hicho ni kukuza mashirikiano yaliyopo kati ya JMT na Taasisi hiyo hasa katika kuiwezesha Tanzania kupata msaada wa kifedha na utalaamu wa kiufundi katika kuisadia nchi kupata fedha za kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Katika mkutano huo, Dkt. Muyungi alieleza kuwa Tanzania ikiwa moja ya nchi nufaika na fedha kutoka mfuko huo za utekelezaji miradi ya maendeleo ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Hivyo, kutokana na fursa ilizopo Tanzaia imeweza kuwasilisha maombi ya kuipatia Ithibati Wizara ya Fedha ili kuweza kupata fedha moja kwa moja kutoka katika mfuko huo.
Hadi sasa JMT inataasisi moja ambayo ni CRDB iliyopewa ithibati ili kuweza kunufaika moja kwa moja na fedha zinazotolewa na mfuko huo za kuhimili athari za abadiliko ya tabiachi.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Wizara ya Fedha na Taasisi za Kifedha za nchini ikiwemo Benki ya TIB, Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) na Benki ya NBC.



