Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Naibu Waziri Kwagilwa aalika wadau kukijanisha Tanzania

Jun, 17 2026

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa amewaomba wadau wa maendeleo kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kupanda miti ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na watendaji wa Benki ya NMB kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kuweka mikakati ya pamoja ya hifadhi ya mazingira endelevu, kikao kimefanyika jijini Dodoma Juni 16, 2026.

Mhe. Kwagilwa alisema kuwa katika kufikia lengo la upandaji wa miti takriban bilioni mbili lililowekwa kupitia Dira 2050 zinahitajika nguvu za pamoja kati ya Serikali na wadau na kuendelea kuhamasisha jamii kupanda miti kwenye maeneo yao.

Alisema ni lazima kuunganisha nguvu za pamoja kushirikiana ili kuifanya nchi kuwa ya kijani kwani hata katika kaulimbiu iliyotumika kwenye Siku ya Mazingira Duniani mwaka huu inasema ‘Dira 2050; Tuwajibike kukijanisha Tanzania’ ambayo inasisitiza umuhimu wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

“Karibu nusu ya eneo la nchi yetu ni misitu, tunaongelea hekta takriban milioni 48 na hata tungeweza kuwa zaidi ya hapo lakini bado tunakata sana misitu, na ukitembea huioni miti pamoja na kufanyika kampeni nyingi, natamani tupande miti zaidi,” alisisitiza.

Aidha, Mhe. Kwagilwa alipendekeza kuwepo na vitalu vya miche katika kata zote 3950 zilizopo nchini ambayo ikisambazwa na kupandwa hatua hiyo itasaidia kustawisha miti mingi zaidi na kupunguza changamoto ya upotevu wa miti 370,000 inayopotea kila mwaka.

Pamoja na hayo alisema kwenye Sheria mpya ya Mazingira itakuwa ni vyema ikaweka sharti la kumtaka mtu mwenye kumiliki eneo kubwa ni lazima apande miti badala ya kuliacha likawa wazi bila kutumika.

Kuhusu kaboni ya buluu aliipongeza Beki ya NMB kwa kuanza kutekeleza miradi hiyo katika ukanda wa pwani ambapo aliwaomba wakutane na wataalamu wa Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni (NCMC) chini ya Ofisi ya Makamau wa Rais kwa ajili kubadilishana uzoefu na kufanikisha jambo hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Biashara ya Serikali NMB Bi. Vicky Bishubo alisema pamoja na masuala mbalimbali, Benki hiyo imejikita katika shughuli za mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Alisema katika kuunga mkono juhudi hizo, mwaka 2024 walizindua kampeni ya upandaji wa miti nchi nzima kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), halmashauri kupitia shule za Tazania Bara na Zanzibar na taasisi zikiwemo Magereza na Jeshi la Wananchi kwa kupanda miti milioni mbili.

Bi. Vicky alisema asilimia 80 ya miti iliyopandwa ilistawi hivyo wanafunzi waliofanya vizuri katika ustawishaji wa miti walipata zawadi kama motisha na kuongeza kuwa lengo ni kupanda miti milioni 10 ifikapo mwaka 2030.

Naye Meneja Mkuu wa NMB Foundation Bw. Nelson Karumuna alisema katika uchumi wa buluu, taasisi hiyo inatekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wakulima wa mwani katika eneo la pwani ili waongeze kipato na kutunza maeneo ya bahari.

Aliongeza kuwa taasisi hiyo inashiriki kikamilifu katika kupunguza hewa ya ukaa ambapo inatarajia kuzindua mradi wa vyombo vya moto (magari) vinavyotumia umeme badala ya mafuta.

Habari

Settings