Idara ya Muungano

Idara hii imekasimiwa majukumu ya kuratibu mambo ya Muungano; na kuratibu ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mambo yasiyo ya Muungano. Idara inaongozwa na Mkurugenzi wa Muungano na imegawanyika katika Sehemu kuu tatu (3) ambazo ni:-

(i). Sehemu ya Jamii na Siasa;

(ii). Sehemu ya Uchumi na Fedha; na

(iii). Ofisi ya Zanzibar

Bi. Hanifa Selengu


Mgawanyo wa majukumu hayo upo katika sehemu kuu tatu kama ifuatavyo: -

a) Sehemu ya Jamii na Siasa

Sehemu hii inatekeleza kazi zifuatazo: -

(i). Kuratibu vikao vya Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ ya Kushughulikia Masuala ya Muungano kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wa changamoto za Muungano;

(ii). Kutoa ushauri wa kitaalamu wa kijamii na kisiasa kwa masuala yanayohusu Muungano;

(iii). Kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya Muungano na yasiyo ya Muungano;

(iv). Kuratibu uandaaji wa taarifa ya mwaka ya hali ya utekelezaji wa masuala ya Muungano; na

(v). Kufanya utafiti kuhusu masuala ya kijamii na kisiasa yanayohusu masuala ya Muungano.

b) Sehemu ya Uchumi na Fedha

Sehemu hii inatekeleza kazi zifuatazo:-

(i). Kuchambua na kushauri kuhusu sera za uchumi na fedha zinazohusu masuala ya Muungano;

(ii). Kufanya ufuatiliaji wa miradi ya kiuchumi na kijamii inayotekelezwa pande zote za Muungano;

(iii). Kufanya utafiti kuhusu masuala ya uchumi na fedha yanayohusu masuala ya Muungano;

(iv). Kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya uchumi na fedha yanayohusu masuala ya Muungano;na

(v). Kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa maagizo mbalimbali ya Muungano na yasiyo ya Muungano

c) Ofisi ya Zanzibar

Sehemu hii inatekeleza kazi zifuatazo:-

(i). Kutoa huduma kwa Mhe. Makamu wa Rais katika upande wa Zanzibar na kuratibu masuala ya Muungano;

(ii). Kuwa kiungo kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuhusu masuala yasiyo ya Muungano;

(iii). Kuratibu masuala ya rasilimali watu na utawala; na

(iv). Kusimamia majengo, kuratibu shughuli za kila siku na kusimamia masuala ya fedha na manunuzi

Settings