Bw. Edwin Makamba
1)Kuchambua na kumshauri Makamu wa Rais katika masuala ya kijamii, kisheria, mazingira siasa na uchumi;
2)Kuandaa ratiba ya kazi za Makamu wa Rais;
3)Kutoa taarifa na kufuatilia utekelezaji wa maelekezo ya Makamu wa Rais katika Wizara za Kisekta, Taasisi na Mamlaka za Serikali za Mitaa;
4)Kuchambua taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Makamu wa Rais kutoka katika Wizara za Kisekta, Taasisi na Mamlaka za Serikali za Mitaa na kumshauri Makamu wa Rais kuhusu;
5)Kuandaa hotuba ya Makamu wa Rais;
6)Kupanga na kuratibu mahojiano na mijadala ya Makamu wa Rais; na
7)Kusimamia makazi ya Makamu wa Rais.