Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
Kitengo kinaundwa na Mkaguzi wa Ndani Mkuu
Bi. Mwatano Maganga
Lengo
Kutoa huduma za ushauri kwa Afisa Masuhuli kuhusu matumizi sahihi ya rasilimali
Kitengo hiki kinatekeleza majukumu yafuatayo:-
- (i). Kukagua na kutoa taarifa kuhusu mapokezi na utunzaji wa fedha na matumizi ya mali na fedha za Serikali;
- (ii). Kuangalia Ufanisi na Ukamilifu katika utekelezaji wa Sheria na Kanuni za Fedha.
- (iii). Kujiridhisha kwa uwepo wa udhibiti wa kutosha katika mifumo ya fedha na ile ya utendaji kwa lengo la kuongeza tija; na
- (iv). Kukagua na kutoa taarifa juu ya uainisho sahihi wa vifungu vya mapato na matumizi ya fedha za Serikali.