Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu
Idara inaongozwa na Mkurugenzi
Bw. Paul Masanja
Lengo
Kutoa huduma za usimamizi wa rasilimawatu na utawala katika Ofisi.
Majukumu
- Kusimamia shughuli zote za Rasilimaliwatu katika Ofisi kama vile Kamati mbalimbali za ajira, mafunzo, mpango wa kurithishana madaraka (Succession Plan),
- Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Sheria; Kanuni na Taratibu za Uendeshaji wa kazi ndani ya Ofisi;
- Kuratibu masuala ya usalama wa vifaa, majengo na watumishi kazini
- Kusimamia masuala ya jinsia, Kudhibiti Ukimwi na Mikakati ya Kupambana na Rushwa Kutafsiri Kanuni za huduma za umma, Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma (Standing Order) na sheria zingine za kazi;(ii). Kusimamia uhusiano mzuri wa wafanyakazi na ustawi pamoja na afya, usalama, michezo na utamaduni;(iii). Kutoa usajili, kuweka kumbukumbu za ofisi na huduma za wahudumu;
Kusimamia masuala ya kanuni;(iv). Kutoa huduma za ulinzi, usafiri na mambo mengine ya kiutawala kwa ujumla; (v). Kutekeleza mambo mbalimbali ikiwemo Anuai za Jamii, Wasiojiweza, Wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI;(vi). Kusimamia jukumu la utekelezaji wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa Ofisi.
Idara inaundwa na Sehemu mbili (2):-
- Sehemu ya Utawala
- Sehemu ya Rasilimaliwatu.
1:Sehemu ya Utawala
Majukumu ya Sehemu hii ni kama ifuatavyo:-
- (i). Kutafsiri Kanuni za huduma za umma, Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma (Standing Order) na sheria zingine za kazi;(ii). Kusimamia uhusiano mzuri wa wafanyakazi na ustawi pamoja na afya, usalama, michezo na utamaduni;(iii). Kutoa usajili, kuweka kumbukumbu za ofisi na huduma za wahudumu;
Kusimamia masuala ya kanuni;(iv). Kutoa huduma za ulinzi, usafiri na mambo mengine ya kiutawala kwa ujumla; (v). Kutekeleza mambo mbalimbali ikiwemo Anuai za Jamii, Wasiojiweza, Wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI;(vi). Kusimamia jukumu la utekelezaji wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa Ofisi.
Sehemu hii inaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.
2:Sehemu ya Rasilimaliwatu
Majukumu ya Sehemu hii ni kama ifuatavyo:-
- (i). Kusimamia zoezi zima la ajira ikiwemo kukusanya, kuchagua, kuchukua, kuthibitisha kazini pamoja na uhamisho;(ii). Kusimamia maendeleo na mafunzo ya rasilimali watu;(iii). Kuratibu mafunzo ya awali na programu za utangulizi kwa waajiriwa wapya;(iv). Kuweka mipango ya rasilimali watu ili kujua mahitaji na idadi ya wataalamu walio chini ya Ofisi; (v). Kusimamia mishahara na kuandaa idadi ya watu wote walioajiriwa;(vi). Kusimamia utekelezaji wa malengo na mfumo wa wazi wa kupima utekelezaji wa watumishi wa Ofisi.
Sehemu hii inaundwa na Mkurugenzi Msaidizi.