Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Dkt. Dugange awaomba wananchi waitunze miradi

Mar, 12 2026

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange amewataka wananchi waitunze miradi inatekelezwa katika vijiji vyao ili iendelee kuleta tija.

Amesema hayo wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira ya kukagua Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bayoanuai Tanzania (SLR) katika Halmashauri ya Iringa.

Dkt. Dugange alisema Serikali inatumia fedha nyingi ili kuwaletea wananchi miradi hiyo ambayo inawezesha kufanya shughuli za kujiingizia kipato badala ya kuharibu mazingira.

Aliwataka wananchi hao kuhakikisha hawakati miti hovyo kwa ajili ya kuni na mkaa ili kujipatia kipato hivyo badala yake waitumie miradi hiyo kujikwamua kiuchumi huku wakitunza mazingira.

Alisema hayo wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi wa ujenzi wa jengo la kiwanda kidogo cha kuchakata mahindi katika Kijiji cha kipera, wenye thamani ya shilingi milioni 116.6 ambao umefikia asilimia 75 wakati ujenzi ukiendelea.

Faida ya mradi huo ni kuwaondoa kwenye kazi ya awali iliyokuwa na uharibifu wa mazingira, kujifunza na kufanya kazi mbadala ya kuingiza kipato, kutoa huduma ya kuongeza thamani ya mahindi yanayolimwa kwenye kijiji hicho.

Aidha, uwepo wa jengo la kuhifadhi mahindi na unga pamoja na mashine kutachechemua uchumi kwenye kijiji kwa kupata masoko ya mahindi ya wanakijiji kwenye mashine lakini pia unga ulioandaliwa kisasa utapata soko kwa urahisi.

Sanjari na hilo, pia wanakijiji watanufaika na shughuli mbalimbali zilizoongezeka kwenye mnyororo wa thamani wa zao la mahindi kama upatikanaji wa pumba za mifugo, biashara ya huduma za fedha eneo la kiwanda.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Festo Kiswaga alisema Serikali itaendelea kutekeleza na kukamilisha miradi iliyoahidi.

Kuhusu biashara ya kaboni aliwataka wananchi waendelee kuwa na imani na Serikali kwani kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais itaweka mazingira wezeshi ya uwekezaji ili kufahakisha mradi wa

Mhe. Kiswaga alisema kuwa Serikali inataka kuona wananchi wanapata matunda ya nguvu zao za kuhifadhi mazingira yaani misitu inayowazunguka kwa kutokata miti ovyo kwa ajili ya kuni, mkaa na shughuli zingine.

Katika hatua nyingine, wajumbe hao walitembelea kituo cha kukusanyia maziwa katika kijiji cha Ilalasimba, mradi uliokuja baada ya mwekezaji ASAS kuona mafanikio ya wananchi 200 kuanzisha ufugaji wa ng’ombe wa maziwa kama shughuli mbadala na kuondokana na uharibifu wa mazingira.

Miongoni mwa faida za mradi ni kuwa umejenga uchumi mpya kijijini kwa kuwa na soko la maziwa la uhakika, kuongezeka kwa mapato kwenye kaya na hivyo kujikimu kimaisha na kuwa na kipato cha uhakika kwani mahitaji ya maziwa ASAS kama malighafi bado ni makubwa.

Mradi wa SLR unatekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) katika halmashauri za Wilaya za Iringa, Wanging’ombe, Mbarali na Mbeya katika bonde la Ruaha Mkuu na halmashauri za Sumbawanga, Mpimbwe na Tanganyika katika Bonde la Ziwa Rukwa.

Lengo la mradi ni kuboresha maisha ya jamii kupitia urejeshaji jumuishi wa ardhi na misitu iliyoharibika kwa kunufaisha zaidi ya kaya 100,000 zinzaokadiriwa kuwa na wakazi 400,000 wa makundi mbalimbali ya kiuchumi.

Habari

Settings