Idara ya Sera na Mipango
Idara inaongozwa na Mkurugenzi
Bw. Ignas Chuwa
Idara hii ina majukumu yafuatayo;
Idara ya Sera na Mipango inasimamiwa na Mkurugenzi akisaidiwa na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mipango na Bajeti na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Ufuatiliaji na Tathmini. Idara hii ina majukumu yafuatayo·
- (i). Kusimamia uandaaji na utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Muda wa Kati wa Ofisi.
- (ii). Kuratibu maandalizi ya Bajeti na Hotuba ya Ofisi pamoja na kuratibu ushiriki wa Wizara katika vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- (iii). Kuratibu uandaaji wa taarifa za utekelezaji wa bajeti ya Ofisi.
- (iv). Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mipango, bajeti na miradi ya maendeleo ya Ofisi na taasisi zilizo chini yake.
- (v). Kuratibu utunzaji wa takwimu mbalimbali za Ofisi.
- (vi). Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Idara na Taasisi zilizo chini ya Ofisi katika masuala ya uandaaji wa mipango, bajeti na taarifa za utekelezaji.
Idara hii inaundwa na Sehemu mbili (2) kama ifuatavyo:-
- Sera, Utafiti na Ubunifu
- Sehemu ya Mipango na Bajeti
1:Sera, Utafiti na Ubunifu
Sehemu hii ina majukumu yafuatayo:-
- ·Kuratibu maendeleo na utekelezaji wa sera za Wizara;
- Kuratibu mapitio ya sera za Mawaziri; Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa Sera za Wizara;
- Kupitia na kushauri juu ya karatasi za sera zilizoandaliwa na Wizara nyingine; Kuandaa miongozo ya masuala ya utafiti na uvumbuzi kwa Wizara;
- Kuratibu masuala ya utafiti na uvumbuzi kwa ajili ya kufanya maamuzi sahihi;
- Kuratibu usimamizi wa masuala ya ubunifu kwa Wizara;
- Kushirikiana na taasisi za utafiti za kitaifa na kimataifa na vituo vya data kwa madhumuni ya kukusanya na kubadilishana taarifa za utafiti na uvumbuzi;
- Kuainisha maeneo ya utafiti na vipaumbele vya Wizara;
- Kuandaa mikakati ya utekelezaji na usambazaji wa matokeo ya utafiti.
- Sehemu hii inaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.
2: Mipango na Bajeti
Sehemu hii na majukumu yafuatayo:-
- ·
(i). Kuratibu maandalizi na mapitio ya Sera ya Taifa ya Mazingira na kuwianisha na Sera nyingine za Kitaifa;
- (ii). ii.Kuratibu utoaji wa maoni na ushauri kuhusu Sera na Nyaraka za Baraza la Mawaziri zilizoandaliwa na Wizara nyingine.
- (iii). Kuandaa (Memorandum of Understanding) za miradi na programu kwa ajili ya ushirikiano na utafutaji wa fedha;
- (iv). Kuandaa taarifa za utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na maoni ya Kamati za Bunge;
- (v). Kuratibu maandalizi ya hotuba ya mwaka ya mpango wa bajeti wa Ofisi.
- (vi). Kuratibu uandaaji wa mpango wa mwaka na bajeti ya Wizara kwa utekelezaji na mpango mkakati wa muda wa kati;(vii). Kuunganisha taarifa za miradi ya maendeleo, programu na mpango wa utekelezaji;
- (viii). viii.Kuandaa mikakati ya utafutaji fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo;
- (ix). Kutoa miongozo ya kitaalam na kujenga uwezo kwa Wizara kuhusu uandaaji wa mpango mkakati na bajeti. Sehemu hii inaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.