Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Addis kushiriki Mkutano wa Pili wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi za Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaofanyika katika Jiji la Addis Ababa nchini Ethiopia. Tarehe 08 Septemba 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimpokea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Mhe. Kembo Campbell Mohadi alipowasili Ikulu Jijini Dar es salaam akiwa katika ziara ya kikazi nchini Tanzania. Tarehe 30 Agosti 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazungumzo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kambarage mkoani Dodoma tarehe 03 Julai 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amejumuika na viongozi mbalimbali wa Serikali, Dini na Chama katika dua ya pamoja ya kumuombea aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume katika kumbukizi ya miaka 52 ya kifo chake tarehe 07 Aprili 2024 iliyofanyika Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi – Kisiwandui Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ameongoza viongozi na wananchi kuaga mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam tarehe 13 Februari 2024.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango amepokea vifaa tiba kwa ajili ya Watoto Njiti kutoka Taasisi ya Doris Mollel na vifaa tiba kutoka Tume ya Taifa ya Ushindani katika Hospitali ya Wilaya ya Buhigwe, Kigoma Julai 06, 2023.