Idara ya Mazingira

Idara inaongozwa na Mkurugenzi

Bi. Kemilembe Mutasa

Majukumu

Sehemu hii inaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.

2: Sehemu ya Udhibiti wa Uchafuzi wa Mazingira

(i). Kuandaa, kupitia na kusimamia na kutathmini utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni, Miongozo na Mikakati zinazohusu Udhibiti wa Uchafuzi wa Mazingira.

(ii). Kufuatilia na kutathimini udhibiti wa uchafuzi wa mazingira uanotokana na shughuli za viwanda, kilimo, usafirishaji, uchimbaji wa madini, nishati n.k;

(iii). Kuandaa, kuratibu na kusimamia utekelezaji wa mikakati na shughuli mbalimbali zinazohusiana na udhibiti wa uchafuzi wa mazingira kwa kushirikiana na Serikali za mitaa na wadau wengine;

(iv). Kuratibu utekelezaji wa mikataba ya kimataifa na ya kikanda inayohusu Udhibiti wa Uchafuzi wa Mazingira. Mikataba hiyo ni: Mkataba wa Vienna na Montreal inayohusu uhifadhi wa Tabaka la Ozoni; Mkataba wa Stockholm unaohusu udhibiti wa kemikali zinazodumu kwa muda mrefu; Mkataba wa Basel unaohusu udhibiti wa usafirishaji wa taka zenye sumu baina ya nchi na nchi na utupaji wake; Mkataba wa Minamata unahusu udhibiti wa matumizi ya zebaki; Mkataba wa Rotterdam kuhusu upashanaji taarifa kuhusu baadhi ya kemikali hatarishi za viwandani na viuatilifu katika biashara ya kimataifa (Rotterdam Convention on prior informed consent procedure on hazardous chemicals and pesticides in International trade) na Mkataba wa Bamako unahusu kuzuia uingizaji wa taka za sumu barani Afrika na kuthibiti usimamizi wake.

(v). Kuratibu utoaji elimu kwa umma kuhusu masuala yanayohusu udhibiti wa uchafuzi wa mazingira

(vi). Kuandaa na Kutekeleza Miradi ya Mazingira inayohusu udhibiti wa uchafuzi wa mazingira.

Sehemu hii inaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.

3: Sehemu ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi

(i). Kuandaa na kupitia Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo;
(ii). Kuratibu taratibu za Tathmini ya Athari kwa Mazingira katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo;
(iii). Kuratibu taratibu za Tathmini ya Mazingira Kimkakati katika uanzishwaji wa Sera, Sheria, Kanuni, Mikakati, Programu na Mipango;
(iv). Kuandaa programu na mikakati mbalimbali ya hifadhi ya mazingira;
(v). Kusimamia na kuratibu Mkataba wa kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, Mkataba wa kimataifa wa kudhibiti kuenea kwa hali ya jangwa na ukame pamoja na miradi mbalimbali ya kudhibiti uharibifu wa mazingira;
(vi). Kuratibu shughuli za mahusiano ya nchi na taasisi zingine katika eneo la mazingira. Taasisi hizi ni pamoja na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu (CSD) na Kamati ya Mawaziri wa Afrika kuhusu Mazingira (AMCEN); na
(vii). Kuratibu utekelezaji wa Mikataba ya Kimataifa na Kikanda kuhusu: Mabadiliko ya Tabianchi na Itifaki ya Kyoto na Makubaliano ya Paris; Kuzuia kuenea kwa hali ya jangwa na ukame; Itifaki ya SADC kuhusu usimamizi endelevu wa mazingira na maliasili; na Itifaki ya Afrika Mashariki kuhusu mazingira na maliasili.

Sehemu hii inaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.

Settings