Dkt. Juma Mohamed Salum
Idara hii imekasimiwa majukumu ya kuratibu mambo ya Muungano; na kuratibu ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mambo yasiyo ya Muungano na majukumu yake ni: Kutoa huduma kwa Mhe. Makamu wa Rais katika upande wa Zanzibar na kuratibu masuala ya Muungano;
2)Kuwa kiungo kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuhusu masuala yasiyo ya Muungano;
3)Kuratibu masuala ya rasilimali watu na utawala; na
4)Kusimamia majengo, kuratibu shughuli za kila siku na kusimamia masuala ya fedha na manunuzi.
Mgawanyo wa majukumu hayo upo katika sehemu kuu tatu kama ifuatavyo: -
a)Sehemu ya Jamii na Siasa
Sehemu hii inatekeleza kazi zifuatazo: -
1)Kuratibu vikao vya Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ ya Kushughulikia Masuala ya Muungano kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wa changamoto za Muungano;
2)Kutoa ushauri wa kitaalamu wa kijamii na kisiasa kwa masuala yanayohusu Muungano;
3)Kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya Muungano na yasiyo ya Muungano;
4)Kuratibu uandaaji wa taarifa ya mwaka ya hali ya utekelezaji wa masuala ya Muungano; na
5)Kufanya utafiti kuhusu masuala ya kijamii na kisiasa yanayohusu masuala ya Muungano.
a)Sehemu ya Uchumi na Fedha
Sehemu hii inatekeleza kazi zifuatazo:-
1)Kuchambua na kushauri kuhusu sera za uchumi na fedha zinazohusu masuala ya Muungano;
2)Kufanya ufuatiliaji wa miradi ya kiuchumi na kijamii inayotekelezwa pande zote za Muungano;
3)Kufanya utafiti kuhusu masuala ya uchumi na fedha yanayohusu masuala ya Muungano;
4)Kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya uchumi na fedha yanayohusu masuala ya Muungano;na
5)Kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa maagizo mbalimbali ya Muungano na yasiyo ya Muungano
a)Ofisi ya Zanzibar
Sehemu hii inatekeleza kazi zifuatazo:-
1)Kutoa huduma kwa Mhe. Makamu wa Rais katika upande wa Zanzibar na kuratibu masuala ya Muungano;
2)Kuwa kiungo kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuhusu masuala yasiyo ya Muungano;
3)Kuratibu masuala ya rasilimali watu na utawala; na
4)Kusimamia majengo, kuratibu shughuli za kila siku na kusimamia masuala ya fedha na manunuzi.