Maktaba ya Picha

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ashiriki zoezi la kupiga kura ya kuchagua Rais, Mbunge na Diwani akiwa katika Kijiji cha Kasumo, Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma leo tarehe 29 Oktoba 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameungana na Viongozi, Waumini pamoja na Wananchi mbalimbali katika Ibada ya kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu. Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Francisko wa Asizi, Mwanjelwa Mkoani Mbeya tarehe 14 Oktoba 2025. Ibada hiyo imeongozwa na Akofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mbeya Mhashamu Gervas Nyaisonga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia Mkutano wa Pili wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Addis (AICC) Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia. Tarehe 08 Septemba 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizindua Kituo cha Upandikizaji Figo kilichopo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma tarehe 03 Septemba 2025.
Settings