Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Kitengo kinaongozwa na Mkuu wa Kitengo

Bi. Sarah Kibonde

Lengo

Kutoa huduma za habari, mawasiliano na kuwa kiunganishi kati ya Ofisi na umma kupitia vyombo vya habari.

Majukumu ya Kiting ni kama ifuatavyo:-

  • (i). Kutayarisha na kutekeleza Mkakati wa Mawasiliano wa Ofisi;
  • (ii). Kuratibu uandaaji, utoaji na usambazaji wa Makala za Kisekta na Kiofisi kwa ajili ya warsha, semina na mikutano na vyombo vingine vya habari;
  • (iii). Kutoa elimu kwa umma juu ya masuala mtambuka yanayohusu Ofisi kupitia magazeti, redio, luninga, mitandao ya kijamii pamoja na maeneo mbalimbali;
  • (iv). Kuhuisha tovuti ya Ofisi kwa kuweka kwa wakati taarifa mbalimbali zinazohusu Ofisi;
  • (v). Kujibu hoja na kutolea ufafanuzi, malalamiko na kero mbalimbali zinazotolewa na wananchi kupitia vyombo vya habari.
Settings