Kitengo cha Huduma za Sheria
Kitengo kinaongozwa na Mkurugenzi
Bw. Dustan Shimbo
Lengo
Kutoa utaalamu wa huduma za kisheria katika Ofisi
Kitengo kinatekeleza majukumu kama ifuatavyo:-
- (i) Kutoa msaada wa kisheria kwa Ofisi na Taasisi zake katika kutafsiri sharia, na makubaliano mengine ya kisheria;
- (ii) Kutoa ushauri wa kitaalamu katika maandalizi ya nyaraka za kisheria kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwakasheria Mkuu wa Serikali;
- (iii) Kuchambua na kushauri kuhusu sharia, kanuni na miongozo inayohusu masuala ya Muungano na yasio ya Muungano;(iv) Kushiriki katika mashauriano na mikutano ya kisheria inayohusu Mazingira, Muungano na masuala yasiyo ya Muungano;
- (v) Kutafsiri sheria kuhusu masula ya Mazingira;
- (vi) Kusikiliza mashauri ya jinai na madai yanayohusu Ofisi kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali; na (vii) Kufuatilia, kutathmini na kutoa taarifa ya utekelezaji wa maamuzi ya mahakama kuhusu mashauri yanayohusu Ofisi katika masuala ya Muungano na yasiyo ya Muungano.