Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Dkt. Muyungi ahimiza kasi ujenzi wa jengo la OMR, Mtumba Dodoma

Mar, 09 2026

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya Suma JKT kuongeza kasi ya ujenzi wa Jengo la Ofisi hiyo unaoendelea katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.

Dkt. Muyungi amesema hayo Machi 09, 2026 wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Ofisi hiyo ambapo aliongozana na Viongozi na Menejimenti kwa ajili ya kujionea na hatua iliyofikiwa katika mradi huo.

Amesema mkandarasi wa kampuni ya Suma JKT hana budi kufanya kazi masaa 24 ili kuwezesha maboresho na ukarabati wa baadhi ya maeneo ndani ya jengo ambayo hayajakamilika.

Ameongeza kuwa Ofisi yake haitongeza muda wa kukamilisha mradi huo kwa kuwa ilishafanya hivyo hapo awali na hivyo kumtaka mkandarasi hukakikisha anatumia vyema muda uliopo kuweza kukamilisha na kukabidhi jengo hilo.

“Kamati ya Bunge inatarajia kufanya ziara katika mradi wa jengo hili tarehe 18 Machi mwaka huu, hivyo nawasisitiza kuhakikisha mnakamilisha kazi hii kwa wakati kabla ya tarehe hiyo kufika” amesema Dkt. Muyungi.

Aidha Dkt. Muyungi amesema Ofisi yake imetimiza mahitaji yote yaliyohitajika kwa ajili ya kukamilisha mradi wa ujenzi wa jengo hilo ikiwemo malipo ya fedha kwa mkandarasi na ununuzi wa samani mbalimbali.

Pia Dkt. Muyungi amemtaka mkandarasi huyo kuhakikisha anajenga miundombinu yenye mifumo ya kisasa ya uchakataji na usimamizi wa taka ngumu kuweza kutumia katika jengo hilo pindi litakapokamilika hatua inayolenga kutunza mazingira.

Katika ziara hiyo Dkt. Muyungi aliongozana na Naibu Katibu Mkuu (Muungano), Bw. Abdallah Hassan Mitawi na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira), Mhe. Balozi Baraka Luvanda pamoja na menejementi ya ofisi hiyo.

Habari

Settings