Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Katibu Mkuu Dkt. Muyungi akagua miradi ya maendeleo Wilaya ya Nyasa

Jul, 16 2026

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi amefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma leo Julai 16, 2026.

Miongoni mwa miradi aliyokagua ni pamoja na mradi wa kizimba cha ufugaji wa samaki kilichopo katika Kijiji cha Hinga ambao utasaidia kupanuka wigo wa uvuvi hivyo kuchochea sekta ya uchumi wa buluu.

Pia, mradi huo unatarajiwa kuwezesha ufugaji wa samaki kuanzia 15,000 hadi 21,000 ambao ni wastani wa samaki tani nne baada ya miezi sita hivyo kuongeza kipato cha wafugaji na halmashauri hiyo kwa ujumla.

Mradi mwingine aliotembelea Dkt. Muyungi ni ujenzi wa bandari ya Mbamba Bay ambaa ukikamilika utaunganishwa na bandari ya Mtwara kwa ajili ya kusafirisha mizigo kwenda nchi jirani.

Faida nyingine ni kuwa makao makuu yaa bandari ya Nyasa yatahamishiwa bandari ya Mbamba Bay baada ya kukamilika kwa mradi na hivyo kuongeza mapato ya Serikali.

Akizungumza mara baada ya kutembelea miradi hiyo kwa nyakati tofauti Katibu Mkuu huyo alisema itakuwa chachu katika kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi.

“Ofisi ya Makamu wa tuna kazi ya kusimamia mazingira na kama mnavyofahamu changamoto ya mabadiliko ya tabianchi inaaathiri maziwa yetu kwa mfano ongezeko upungufu wa maji hivyo tunapotekeleza miradi hii tuone tunatokaje katika kukabiliana nayo,” alisema.

Habari

Settings