Waziri Jafo aelekeza mitaro isafishwe

Sep, 19 2023

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amezitaka taasisi na wamiliki wa majengo yanayopakana na mitaro kuisafisha ili kuweka maeneo hayo katika hali ya usafi.

Ametoa maelekezo hayo wakati wa Maadhimisho ya Usafi Duniani iliyofanyika katika eneo la Mbagala Zakhem wilayani Temeke Mkoa wa Dar es Salaam Septemba 19, 2023.

Akiongoza viongozi na wananchi katika zoezi la usafishaji wa mitaro, Dkt. Jafo amesema wamiliki wa majengo au taasisi zilizopo katika majengo hayo zina jukumu la kuhakikisha inakuwa safi.

Amewataka wamiliki hao pia kuhakikisha taka hazitupwi katika mitaro hiyo ili kupisha maji ya mvua kupita kwa urahisi kuelekea katika mashimo na kutosababisha mafuriko.

Settings