Habari
Makamu wa Rais afanya mazungumzi na Balozi Gagauti
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Mteule wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Balozi Meja. Jen. Marco Elisha Gaguti.
Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 01 Julai 2026.
Aidha, mazungumzo hayo yamefanyika kufuatia, Mhe. Balozi Gaguti, kufika kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kumuaga akielekea katika Kituo chake cha kazi nchini Uganda, mara baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.



