Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Tanzania, Djibouti zaseka mikakati biashara ya kaboni

Mar, 25 2026

Tanzania kupitia Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni (NCMC) na Djibouti kupitia tasisi inayoratibu masuala ya Kaboni ya nchi hiyo ya Africa Sovereign Carbon Registry (ASCR) Foundation, zimeanza mazungumzo ya ushirikiano wa kimkakati katika biashara ya kaboni inayohusiana na sekta za usafiri wa anga na majini.

Ushirikiano huo unalenga kuhakikisha kuwa sekta zinazochafua zaidi mazingira, hususan mashirika ya ndege na kampuni za usafirishaji, zinachangia moja kwa moja katika ufadhili wa miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi barani Afrika.

Akizungumza wakati wa majadiliano hayo Machi 25, 2026 jijini Dodoma, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Richard Muyungi amebainisha kuwa Tanzania imedhamiria kujifunza mfumo huo kutoka Djibuti kwa kuwa Tanzania inayo bandari kubwa ya Dar es Salaam na Tanga pamoja na viwanja vya ndege vya kimataifa, ambapo vinatarajiwa kuunganishwa na mfumo huo ili kuimarisha ushirikiano wa kikanda.

Ushirikiano huo unaweza kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara ya kaboni ya usafiri wa anga na majini Afrika. Aidha, amefafanua kuwa hatua ya kushirikiana katika biashara ya kaboni ya Usafiri wa aga na majini inalenga kuimarisha nafasi ya Afrika katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuhakikisha mapato yanayotokana na biashara ya kaboni yanabaki barani Afrika.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa ASCR, Mhe. Balozi Ahmed Araita Ali amesema Djibouti tayari imeanzisha mfumo wa bei ya kaboni kwa meli zinazotumia bandari zake, unalazimisha kampuni za usafirishaji kuripoti na kulipia uzalishaji wa kaboni kwa uwazi, kwa mujibu wa kanuni za kimataifa.

Amesisitiza kuwa Mapato yanayotokana na mfumo huo yamekuwa yakitumika kufadhili miradi ya nishati safi, Uhifadhi wa misitu na fukwe.

Amesisitiza kuwa Djibuti imekusudia kuzihamasisha nchi nyingine za Afrika, taasisi za kikanda na wadau wa maendeleo kushirikiana ili kuunda mfumo wa kaboni wa pamoja, wenye uwazi na uaminifu, utakaowezesha Afrika kuzungumza kwa sauti moja katika biashara ya kaboni.

Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni (NCMC) kimeanzishwa Kwa mujibu wa Kifungu cha 29 cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, Sura ya 191 ikiwa ni taasisi ya kimkakati ya kitaifa yenye jukumu la kuratibu shughuli zinazohusiana na na biashara ya kaboni.

Biashara ya Kaboni ni mfumo wa kiuchumi unaoruhusu uuzaji na ununuzi wa Viwango vya Kaboni ambapo lengo lake ni kupunguza gesijoto angani.

Habari

Settings