Serikali yakemea wafanyabiashara wasio waaminifu uingizaji, uzalishaji bidhaa za plastiki

Jun, 02 2023

Serikali imewakemea wafanyabiashara wachache wasio waaminifu wanaoendelea kuingiza, kuzalisha na kusambaza bidhaa za plastiki zisizokidhi viwango zinazotumika kama vifungashio ambavyo zimekuwa chachu ya uchafuzi wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza katika zoezi la usafi wa mazingira katika kuelekea kilele cha Siku ya Mazingira Duniani Juni 5 mwaka huu leo Ijumaa (Juni 2, 2023) Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Antony Mavunde amesema ni wajibu wa Wafanyabiashara kushirikiana na taasisi za Serikali katika kusimamia usitishaji wa Matumizi ya bidhaa za plastiki.

“Kumekuwa na juhudi mbalimbali za Serikali na wadau katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira utokanao na taka za plastiki, hata hivyo bado kuna ukwiukwaji wa sharia kwa baadhi ya wafanyabiashara wanaoingia na kuzalisha mifuko ya plastiki isiyokidhi viwango ambayo inayotumika madukani na watoa huduma” amesema Mhe. Mavunde.

Kwa mujibu wa Mavunde amewaka wananchi kuendelea kuiunga mkono Serikali katika kudhibiti matumizi ya mifuko na bidhaa za plastiki kwa kutoa ushirikiano kwa viongozi wa serikali za mitaaa ili kkurahisisha zoezi hilo la kutokomeza vifungashio visivyokidhi viwango ambavyo vimekuwa visambazwa kupitia njia za panya.

Aidha Mavunde amesema Serikali kupitia Ofisi ya Makamu imeendelea kufanya jitihada kubwa za kuhamasisha suala la utunzaji na uhifadhi wa mazingira katika maeneo ya miji mikuu nchini ikiwemo Jiji la Dodoma, hivyo ni wajibu wa wananchi kuwataka wakazi wa Dodoma na Tanzania kwa ujumla kutosubiri Kilele cha Maadhimisho ya mazingira katika kujishughulisha na suala la usafi katika maeneo yao.

Katika hatua nyingine, Mavunde amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kufanya usafi na kuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku kwa kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi na salama kwa ajili ya ustawi na maendeleo yao ya kijamii na kiuchumi.

Awali akimkaribisha Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Switbert Mkama amesema katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani, Ofisi hiyo imejipanga kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma hatua inayolenga kupendezesha taswira ya Jiji hilo ambalo ni makao makuu ya Serikali.

Kuanzia jana Juni Mosi ambayo tulizindua Wiki ya Mazingira tumeanza kwa kufanya usafi wa mazingira na kupanda miti katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma. Zoezi hili litaendelea hadi siku ya Kilele Siku ya Jumatatu Juni 5 mwaka huu” amesema Dkt. Mkama.

Akitoa salamu za Mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Godwin Gondwe ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amesema Mkoa huo itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuhakikisha kuwa Jiji la Dodoma ambalo ni Makao Makuu ya Serikali linaendelea kuwa safi.

Kilele cha Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo ina kauli mbiu isemayo Pinga Uchafuzi wa Mazingira unaotokana na Taka za Plastiki inatarajia kuwa Juni 5 mwaka huu, ambapo Mgeni rasmi anatarajia kuwa Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango.

Settings