Naibu Katibu Mkuu Mndeme awasili rasmi ofisini

Mar, 19 2024

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme amewasili rasmi katika Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo katika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma kuanza kutekeleza majukumu yake, leo Machi 18, 2024.

Mara baada ya kuwasili katika viwanja vya vya Ofisi hiyo, Bi. Mndeme amepokelewa na Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi na kutambulishwa kwa watumishi na kuwasalimu.

Akizungumza wakati wa kutambulishwa kwa Menejimenti na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga, Naibu Katibu Mkuu Mndeme amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua kushika wadhifa huo.

Bi. Mndeme ameahidi kutoa ushirikiano kwa watendaji hao na kuomba ushirikiano kutoka kwao ili kutekeleza majukumu ya Ofisi hususan katika eneo la Mazingira alilokabidhiwa.

Itakumbukwa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alimuapisha Naibu Katibu Mkuu Mndeme Ikulu jijini Dar es Salaam Machi 13, 2024 akichukua nafasi ya Dkt. Switbert Mkama aliyestaafu utumishi wa umma.

Settings