Naibu Katibu Mkuu Mndeme aapishwa

Mar, 13 2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuapisha Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Machi 13, 2024.

Katika hafla ya uapisho viongozi mbalimbali kutoka Ofisi hiyo wakiwemo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga, katikati ni Naibu Katibu Mkuu (Muungano), Bw. Abdallah Hassan Mitawi na Kaimu Mkurugenzi wa Muungano Bi. Hanifa Selengu na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmni Bw. Sigsbert Kavishe.

Kabla ya uteuzi huo, Bi. Mndeme alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na anachukua nafasi ya Dkt. Switbert Mkama aliyemaliza muda wake wa utumishi kwa mujibu wa sheria.

Mara baada ya uapisho Naibu Katibu Mkuu Mndeme aliwasili katika ofisi ndogo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusaini kitabu na kuzungumza na viongozi mbalimbali.

Settings