Makamu wa Rais awasili Hungary kushiriki Mkutano wa Idadi ya Watu

Sep, 13 2023

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo tarehe 13 Septemba 2023 amewasili Jijini Budapest nchini Hungary ambapo anatarajia kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Tano wa Idadi ya Watu (5th Budapest Demographic Summit) utakaofanyika tarehe 14-15 Septemba 2023.

Mkutano huo wa siku mbili wenye kauli mbiu ya “Dhima ya Familia: Msingi wa Usalama”utahudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali, Watunga Sera, Viongozi wa Taasisi na Mashirika ya Kimataifa, Viongozi wa Dini na Wanataaluma.

Pia Mkutano huo unatarajia kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi baina ya mataifa, uhaulishaji wa teknolojia na uvumbuzi pamoja na ushirikiano katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo.

Settings