Makamu wa Rais ashiriki hafla ya utoaji Tuzo kwa Rais Dkt. Samia

Feb, 04 2025

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameshiriki katika hafla ya utoaji Tuzo ya Kimataifa ya The Global Goalkeepers iliyotolewa na Taasisi ya Gates ya Marekani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Februari 2025.

Tuzo hiyo hutolewa kwa Viongozi waliowezesha nchi zao kuharakisha Maendeleo kuelekea kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Mhe. Rais Samia amepewa tuzo hiyo kwa jitihada za kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano.

Settings