Makamu wa Rais ashiriki hafla ya kupokea Ndege Mpya ya Mizigo

Jun, 03 2023

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ameshiriki katika hafla ya kupokea Ndege Mpya ya Mizigo aina ya Boeing B767-300F iliofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 03 Juni 2023.

Hafla hiyo imeongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Dini, Vyama vya Siasa, Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wasanii, na Wananchi kutoka maeneo mbalimbali.

Settings