Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

VICE PRESIDENT'S OFFICE

News

Makamu wa Rais amuahidi Balozi wa Sweeden Tanzania kuimarisha uhusiano


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania itahakikisha inazidi kuimarisha Uhusiano wake na Sweeden katika Sekta ya Elimu, Uwekezaji wa Biashara, Utalii na Mazingira.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo Januari 17,2020 Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar Es Salaam wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweeden Nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg.

Aidha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amemhakikishia Balozi Sjoberg kwamba Tanzania itaendeleza kukuza na kuimarisha Ushirikiano na Uhusiano kati ya Nchi mbili hizi katika Sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Uwekezaji wa kibiashara na Mazingira wakati Tanzania ikiwa mbioni kuelekea katika Uchumi wa Viwanda.

Nae Balozi wa Sweeden Nchini Tanzania Mhe. Anders Sjoberg amemuahidi Makamu wa Rais kwamba Nchi yake itashirikiana Bega kwa Bega na Tanzania katika kuhakikisha kuwa Nchi mbili hizi zinafikia Malengo.