Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais aelekeza wakulima wa tumbaku wilaya ya namtumbo kulipwa fedha zao

Nov, 11 2026

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ameingilia kati sakata la malipo ya wakulima wa tumbaku katika Kata ya Mgombasi, wilayani Namtumbo, baada ya kubaini kuwa wakulima wa vyama vitano vya ushirika walikuwa wakidai takribani dola za Marekani 849,000 kutokana na tumbaku waliyouza katika msimu uliopita.

Akizungumza mbele ya viongozi wa chama cha ushirika na kampuni ya Three H inayohusishwa na ununuzi wa tumbaku hiyo, akiwa ziarani Wilaya ya Namtumbo Makamu wa Rais ameonyesha kutoridhishwa na kucheleweshwa kwa malipo hayo, akisema hali hiyo inawaathiri wakulima wanaojiandaa kuanza msimu mpya wa kilimo.

Katika maelezo yaliyotolewa, ilibainishwa kuwa chama cha ushirika kilitumia fedha zilizopatikana kutoka kampuni nyingine ya tumbaku, Premium, kulipa sehemu ya madeni ya wakulima, badala ya kuzielekeza fedha hizo katika matumizi yaliyokuwa yamekusudiwa awali.

Makamu wa Rais ameagiza kampuni ya Three H pamoja na viongozi wa chama cha ushirika kwenda katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kusaini makubaliano ya maandishi yatakayobainisha muda wa kukamilisha malipo hayo. “Mimi sitaki stori, Wakulima wanapokwenda shambani hawataki stori, Mwisho wa mwezi huu walipwe fedha zao. Hawajalipwa, hatua za kisheria zitachukuliwa,” amesisitiza.

Aidha, ameelekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchukua hatua endapo makubaliano hayo hayatatekelezwa, huku akimtaka Mkuu wa Wilaya kuhakikisha nakala ya makubaliano hayo inawasilishwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa ajili ya ufuatiliaji. Makamu wa Rais amesema Serikali haitavumilia vitendo vya kuchelewesha malipo ya wakulima au kutumia fedha zinazohusiana na mauzo ya mazao yao katika shughuli nyingine wakati wakulima hao wanahitaji fedha za kujiandaa kwa msimu mpya wa uzalishaji.

Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais ameiagiza Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kuhakikisha unaanza mara moja kununua mahindi kutoka kwa wakulima wa Namtumbo kwa bei ya shilingi 500 kwa kilo, baada ya Serikali kufanya marekebisho ya bei ya awali ya shilingi 450. Amesema bei ya awali ilikuwa ndogo ikilinganishwa na gharama za uzalishaji ambazo kwa baadhi ya wakulima zinaweza kufikia kati ya shilingi 600,000 na 700,000 kwa ekari moja, hali inayopunguza faida na uwezo wao wa kuendelea na shughuli za kilimo.

Makamu wa Rais amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alisikiliza kilio cha wakulima na kuelekeza kufanyika kwa mapitio ya bei hiyo, hatua iliyosababisha kupandishwa hadi shilingi 500 kwa kilo.

Hata hivyo, baada ya wananchi kuonyesha kuwa ununuzi kwa bei hiyo ulikuwa bado haujaanza katika eneo lao, Makamu wa Rais alimhoji Mkurugenzi wa NFRA, Dkt. Komba, na kumtaka kuhakikisha kituo cha ununuzi kinaanza kufanya kazi siku hiyo.

Akijibu maelekezo hayo, Dkt. Komba alisema vifaa vyote muhimu, ikiwemo mizani na mifuko ya kuhifadhia mahindi, vilikuwa vimefikishwa Namtumbo na kwamba ununuzi ungeanza siku hiyo katika ghala la halmashauri linalotumika kwa shughuli hizo. Makamu wa Rais amemtaka Mkurugenzi huyo kuacha timu ya wataalamu itakayosimamia ununuzi na kuhakikisha hakuna watumishi wanaonunua mahindi kwa bei ya chini ili kujinufaisha kwa kuyauza baadaye kwa bei iliyopangwa na Serikali.

“Kazi ya NFRA ni kumlinda mkulima, kuhakikisha kuna usalama wa chakula, lakini pia kuhakikisha bei inakuwa nzuri. Nataka wananchi wa Namtumbo waanze kuuza mahindi yao kwa bei iliyoelekezwa,” amesisitiza.

Makamu wa Rais yuko katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma, akitarajiwa kuelekea Masasi mkoani Mtwara kuendelea na ziara yake ya siku saba katika mikoa ya Kusini.

Habari

Settings