Habari
Biashara ya kaboni kuinufaisha Tanzania kwa mradi wa nishati safi ya kupikia wa Upenergy, Osaka Gas
Tanzania itanufaika na fursa za uwekezaji katika biashara ya kaboni kupitia miradi ya nishati safi ya kupikia inayotekelezwa kwa ushirikiano wa kimataifa chini ya Mfumo wa Ushirikiano wa Viwango Kaboni (Joint Crediting Mechanism – JCM), hatua inayolenga kuvutia mitaji ya kimataifa na kuchochea maendeleo endelevu nchini ya Biashara ya Kaboni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Katika kuendeleza juhudi za Tanzania kunufaika na Biashara ya Kaboni, amekutana na Ujumbe wa Kampuni ya UpEnergy Group na Osaka Group katika mkutano wa kando wa COP 31, jijini Antalya, Uturuki.
Waziri Masauni ameeleza kuwa, Tanzania itanufaika na fursa ya uwekezaji huo kwa kuongeza upatikanaji wa nishati safi kwa kaya, kuchochea upatikanaji wa ajira. Vilevile, mapato yatakayoweza kupatikana kupitia biashara ya Kabaoni.
Kwa upande wa Wajumbe wa Kampuni hiyo, Mjumbe wa Bodi na Mwanzilishi Mwenza wa UpEnergy Group, Bw. Kristian Bruning, akiambatana na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa kampuni hiyo, Bi. Rehema Mbalamwezi, na mshirika wao wa kimkakati kutoka Japan, kampuni ya Osaka Gas, Bw. Nakagawa walibainisha kuwa lengo la kikao hicho ni kuutambulisha mradi wa nishati safi ya kupikia kwa kaya za Kitanzania kupitia Biashara ya Kaboni.
Walifafanua kuwa Osaka Gas ni kampuni ya pili kwa ukubwa nchini Japan katika sekta ya huduma za gesi na nishati, kwa msingi huo imepanga kuwekeza Tanzania katika biashara ya kaboni kupitia sekta ya nishati.
Aidha, ushirikiano huo unatoa fursa kwa NCMC kuimarisha uwezo wa kitaalamu katika masuala ya upimaji, utoaji wa taarifa na uthibitishaji wa upunguzaji wa hewa ukaa (MRV), pamoja na kuhakikisha miradi ya kaboni inazingatia misingi ya uwazi, uadilifu wa kimazingira na manufaa kwa jamii.



