Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Tanzania kunufaika kwa dola milioni 300 za Mfuko wa US-China Green Fund

Nov, 21 2026

Tanzania imefanikiwa kuwa miongoni mwa nchi za kwanza Barani Afrika zitakazo nufaika na uwekezaji wa Mfuko wa US-China Green Fund wenye mtaji wa Dola za Marekani milioni 300, kwa ajili ya kufadhili miradi ya mabadiliko ya tabianchi kupitia biashara ya kaboni.

Maeneo manne ambayo Tanzania itanufaika nayo ni uwekezaji katika urejeshaji wa ardhi ya kilimo, uendelezaji wa mifumo midogo ya umwagiliaji, matumizi ya majiko banifu yanayotumia nishati safi na miradi ya upatikanaji wa maji safi.

Mfuko wa US-China Green Fund utaanza kutekelzwa kwa Awamu ya Kwanza kuanzia January 2027ambapo umetenga Dola za Marekani milioni 300, kwa ajili ya uwekezaji katika miradi ya mabadiliko ya tabianchi kupitia biashara ya kaboni kwa nchi ya China na nchi za Afrika ambapo Tanzania itakuwa ni nchi ya kwanza kunufaika na fedha hizo kupitia Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni NCMC.

Tanzania imefanikiwa kupata fursa hiyo baada ya mkutano wa pembezoni wa Mkutano wa COP31unaoendelea jijini Antalya, Uturuki ulioongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akiwa na Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni-NCMC, Kathryn Kigaraba pamoja na Wataalamu wa NCMC ambapo walikutana na ujumbe wa Climate Neutral Limited pamoja na washirika wake kutoka US-China Green Fund.

Ujumbe wa Mfuko huo uliongozwa na Bw. Atemba Moses, Mkurugenzi Mtendaji wa Climate Neutral Limited, akiambatana na Bw. Keno Xiao, Mshirika wa Uwekezaji (Venture Partner).

Majadiliano yalilenga namna ya kuwezesha upatikanaji wa fedha hizo kwa ajili ya kuendeleza miradi ya kaboni nchini Tanzania kupitia mfumo wa Matokeo ya Upunguzaji wa gesijoto zinazohamishwa Kimataifa (ITMOs).

Waziri alibainisha kuwa Serikali ya Tanzania kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 imeipa sekta ya biashara ya kaboni kipaumbele kama eneo la kimkakati katika kukuza uchumi, kuvutia mitaji na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Alisisitiza kuwa Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imeweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na kuwahimiza wawekezaji kuchukua hatua za kuanzisha na kutekeleza miradi nchini.

Waziri Masauni alifafanua kuwa uwekezaji huo utaleta manufaa kwa wananchi kwa kutoa fursa za ajira, kuimarisha uzalishaji wa kilimo, kuboresha upatikanaji wa nishati safi na maji, pamoja na kuchangia uhifadhi wa mazingira.

Tanzania kupitia Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni, ushiriki wake katika COP31, inaendelea kutafuta washirika wa kimataifa na vyanzo vipya vya fedha vitakavyosaidia kukuza biashara ya kaboni kwa ajili ya maendeleo endelevu kwa taifa na tija kwa wananchi.

Habari

Settings