Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais aipongeza TPDC kwa kuchangisha milioni 500/- matibabu ya moyo kwa watoto

Nov, 21 2026

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amelipongeza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kukusanya Sh milioni 500 kupitia mbio za hisani za TPDC Marathon 2026, na hivyo kuvuka lengo la awali la Sh milioni 200 kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo.

Makamu wa Rais ametoa pongezi hizo aliposhiriki mbio za hisani za Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC Marathon 2026) zilizofanyika jijini Dar es Salaam leo, tarehe 21 Novemba 2026 kwa kaulimbiu “Hatua yako, Okoa Maisha”. Fedha zilizokusanywa zitagharamia upasuaji na matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa watoto waliozaliwa na matatizo ya moyo.

Akizungumza baada ya mbio hizo, Makamu wa Rais amepongeza TPDC na JKCI kwa ushirikiano wao na kuwashukuru wadhamini kwa kuunga mkono juhudi za Serikali. Amesema mpango huo ni sehemu ya wajibu wa Taasisi kwa jamii.

Makamu wa Rais ameitaka TPDC, kuweka lengo la juu zaidi la uchangishaji kwa mbio za mwaka ujao. Pia ameelekeza fedha zote zilizokusanywa zitumike bila kuchelewa kugharamia matibabu ya watoto hao kama ilivyokusudiwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, Balozi Ombeni Sefue, amesema uwajibikaji kwa jamii unapaswa kuwa sehemu ya utamaduni wa uongozi na utendaji wa shirika katika shughuli zake za kila siku.

Balozi Sefue amesema Bodi inatambua wajibu wake wa kuhakikisha kuwa mpango wa kusaidia watoto wenye matatizo ya moyo unasimamiwa ipasavyo. Ameongeza kuwa mpango huo ni sehemu ya wajibu mpana wa TPDC wa kusimamia rasilimali za taifa na kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia thamani ya maisha na ustawi wa wananchi.

Habari

Settings