Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Serikali yaimarisha uratibu wa upandaji, utunzaji wa miti nchini

Nov, 18 2026

Serikali imeendelea kuimarisha juhudi za kuhifadhi mazingira, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuongeza uoto wa asili nchini kupitia mpango wa upandaji na utunzaji wa miti unaohusisha Wizara, taasisi za umma na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Katika kutekeleza azma hiyo, Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Maduhu Kazi amefanya kikao cha pamoja na Wizara na taasisi husika kilichofanyika Novemba 18, 2026, Mtumba jijini Dodoma.

Kikao hicho kinafuatia maelekezo yaliyotolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, mkoani Ruvuma, Novemba 11, 2026, ambapo Wizara na taasisi zilitakiwa kutambua na kutenga maeneo ya kupanda miti, kuchagua aina zinazofaa kwa kuzingatia ushauri wa kitaalamu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), kuanzisha vitalu na kuhakikisha miche inayopandwa inatunzwa.

Dkt. Kazi amesema Serikali inalenga kuweka utaratibu madhubuti wa kuratibu utekelezaji wa zoezi hilo kwa kuzingatia majukumu ya kila taasisi, ili kuhakikisha upandaji miti unakuwa endelevu na wenye matokeo yanayopimika.

Aidha, kikao hicho kimejadili namna ya kutambua na kutenga maeneo yanayofaa kwa upandaji miti, hususan kandokando ya barabara, maeneo ya wazi na maeneo ya taasisi, pamoja na kubainisha aina za miti zinazofaa kulingana na hali ya hewa, udongo na mazingira ya maeneo husika.

Masuala mengine yaliyojadiliwa ni kuimarisha utunzaji wa vitalu vya miti, uzalishaji na usambazaji wa miche bora, pamoja na kuweka utaratibu wa upandaji na utunzaji wa miti ili kuhakikisha inastawi na kuendelea kukua kwa kuhusisha kila mtu.

Vilevile, Serikali inalenga kuunganisha shughuli za upandaji na utunzaji wa miti na miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo maji, barabara, nishati, kilimo na uchimbaji wa madini, pamoja na uwekezaji wa sekta mbalimbali.
Katika kuhakikisha utekelezaji unakuwa na tija, kikao hicho pia kimejadili mifumo ya ufuatiliaji na tathmini itakayowezesha kubaini idadi ya miti iliyopandwa, iliyostawi na hatua zinazochukuliwa kuhakikisha inaendelea kukua.

Habari

Settings