Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Dkt. Muyungi ateta na ujumbe wa viongozi na wataalamu kutoka UNDP

May, 27 2026

Serikali imesema inatambua mchango wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) katika kufanikisha utekelezaji wa miradi ya uhifadhi mazingira na mabadiliko ya tabianchi.

Hayo yamesemwa Mei 26, 2026 Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi wakati wa mazungumzo baina yake na Mshauri wa Kiufundi (Mifumo Ikolojia na Bayoanuai) wa Shirika la UNDP Kanda ya Afrika, Bw. Onesimus Muhwezi.

Dkt. Muyungi amesema ushirikiano na mashirika ya kimataifa ikiwemo UNDP ni muhimu katika kipindi hiki ambacho Serikali imezindua Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ambapo nguzo ya tatu imejumuisha masuala ya mazingira na ustahimilivu wa mabadiliko ya tabianchi.

“UNDP ni mdau muhimu katika utekelezaji wa miradi ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi kwani imeendelea kufanikisha upatikanaji wa fedha katika madirisha ya Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) na mfuko wa dunia wa mabadiliko ya tabianchi (GCF)” amesema Dkt. Muyungi.

Aidha ameeleza kuwa Serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano na Shirika hilo katika kuhakikisha upatikanaji wa fedha za mikopo midogo hatua inayolenga kufanikisha utekelezaji wa miradi ya uhifadhi ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi.

Amesema Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imejipanga vyema ili kuhakikisha inanufaika vyema na fedha zitakazotolewa katika dirisha la 9 la GEF na kufanikisha utekelezaji wa shughuli za uhifadhi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi ili kwenda sambamba na malengo ya Dira 2050.

“Dira 2050 imeweka malengo ya kuhakikisha Tanzania inafikia fursa za uchumi wa kijani sambamba na kuweka mazingira wezeshi katika usimamizi endelevu wa mazingira” amesema Dkt. Muyungi.

Katika hatua nyingine, Dkt. Muyungi amelieleza Shirika la UNDP utayari wa Tanzania kuelekea mkutano wa 12 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Nairobi (COP 12) na kubainisha fursa mbalimbali ambazo Serikali itazipata kupitia mkutano huo na hivyo kuiomba UNDP.

Kwa upande wake Mshauri wa Kiufundi kutoka UNDP, Bw. Bw. Onesimus Muhwezi ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano baina yake na shirika hilo katika utekelezaji wa miradi ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi.

Amesema Shirika hilo litaendelea kutoa kipaumbele kwa Serikali ya Tanzania kuweza kuzifikia na kunufaika na fedha kutoka mfuko wa mazingira wa dunia (GEF) na mfuko wa dunia wa mabadiliko ya tabianchi (GCF).

Mazungumzo baina ya viongozi hao pia yalijikita kujadili mbinu na mikakati ya ushirikiano baina ya Serikali na UNDP katika katika masuala ya usimamizi wa taka, mifumo ikolojia na uhifadhi wa bayoanuai.

Aidha mazungumzo hayo pia yalishirikisha watendaji mbalimbali wa ofisi hizo akiwemo Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa UNDP Tanzania Bw. Amon Manyama.

Habari

Settings