Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Dkt Dugange aihakikishia Kamati ya Bunge kukamilika mradi wa jengo la ofisi

Mar, 18 2026

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange ameihakikishia Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuwa Ofisi hiyo itahakikisha Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi hiyo utakamilika kwa wakati.

Mhe. Dugange amesema hayo Machi 18, 2026 wakati wa ziara ya kamati hiyo ilipotembelea na kukagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi hiyo unaoendelea katika Mji wa Serikali, Mtumba Dodoma.

Dkt. Dugange amesema Ofisi hiyo imekubaliana na mkandarasi wa SUMA JKT kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika kabla au ifikapo Machi 31 mwaka huu ili kuwezesha jengo hilo kutumika na viongozi, watendaji na watumishi wa ofisi hiyo.

“Tumekubaliana na mshauri elekezi na mkandarasi kuwa tunalihitaji jengo kwa haraka ili tuendelee na shughuli zilizopangwa kwa kuwa jengo tunalotumia sasa tumepanga kulikabidhi kwa Kituo cha Taifa cha Kufuatilia Kaboni ambacho kipo Morogoro” amesema Mhe. Dugange.

Ili kufanikisha dhamira hiyo, Dkt. Dugange amesema Ofisi hiyo imefanya tayari imetoa maelekezo kwa Kampuni ya SUMA JKT kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ili maeneo yote yaliyobaki ndani ya ujenzi wa jengo hilo yanakamilika kwa wakati.

Ameeleza kuwa Ofisi hiyo haitokuwa tayari kuongeza muda wa ziara katika mkataba uliopo na hivyo kumtaka mkandarasi wa SUMA JKT kuhakikisha matengenezo yote muhimu ndani ya mradi huo yanakamilika kwa wakati.

Kuhusu suala la uhifadhi wa mazingira ndani ya mradi huo, Dkt. Dugange amesema ofisi hiyo imeweka mifumo ya kisasa ya matumizi endelevu ya nishati mbadala ikiwemo nishati ya jua kama chanzo cha uzalishaji wa umeme ndani ya jengo hilo.

Aidha Dkt. Dugange amesema Ofisi hiyo imepokea maoni, ushauri na mapendekezo ya kamati hiyo na kuahidi kufanyia kazi ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na kuanza kutumika haraka iwezekanavyo.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Edwin Swale ameipongeza Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kusimamia vyema mradi wa ujenzi wa jengo hilo na kumkata mkandarasi SUMA JKT kuhakikisha anafanyia kazi ushauri na maoni ya kamati hiyo.

“Hakikisheni Mradi wa ujenzi Jengo hili unaendana na hadhi na ukubwa wa ofisi na pia nawasihi tuongeze kasi katika kukamilisha kwa wakati kwani taarifa inaonesha fedha za malipo ya ujenzi kwa mkandarasi zimelipwa kwa asilimia kubwa” amesema Mhe. Swale.

Aidha ameeleza Serikali ya Awamu ya Sita imeweka mkazo katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo kutenga fedha za kutosha na kutoa wito kwa wakandarasi kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kuleta tija iliyokusudiwa.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa jengo hilo, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Richard Muyungi amesema mkataba wa ujenzi wa jengo hilo ulisainiwa mwezi Oktoba, 2021 ambapo mkataba huo wa miezi 24 ulipaswa kukamilika tarehe mwezi Novemba, 2023.

Amesema kutokana na kazi hiyo kutokamilika kwa wakati, Mkandarasi aliongezewa muda kwa nyakati tofauti hadi tarehe 30 Machi, 2026 ambapo hadi mradi huo umefikia asilimia 94.5 ya utekelezaji wake.

Habari

Settings