Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Tanzania kupata dola milioni 41 za kuhifadhi wa bioanuwai, kuhimili mabadiliko ya tabianchi

Aug, 08 2026

Tanzania inatarajiwa kunufaika na takribani Dola za Marekani milioni 41 kupitia madirisha mbalimbali ya ufadhili wa Global Environment Facility (GEF), kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi wa bioanuwai, urejeshwaji wa mifumo ikolojia na kujenga ustahimilivu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi.

Hayo yamebainika katika mazungumzo kati ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi na Mratibu wa Bioanuwai wa GEF kwa Afrika, Bw. Jurgis Sapijanskas, yaliyofanyika Nairobi, Kenya, pembezoni mwa mikutano ya SBSTTA-28 na SBI-7 Agosti 07, 2026.

Katika mazungumzo hayo, imeelezwa kuwa takribani Dola za Marekani milioni 16 zimetengwa kupitia dirisha ya GEF – Trust Fund katika Mzunguko wa 9 (GEF-9), huku fursa nyingine zikijumuisha Dola milioni 20 kupitia Mfuko wa Least Developed Countries Fund (LDCF) kwa ajili ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, pamoja na Dola milioni 5 kupitia Mfuko wa Global Biodiversity Framework Fund (GBFF) kwa ajili ya kuendeleza utekelezaji wa vipaumbele vya Taifa vya bioanuwai.

Hivyo, Tanzania inakuwa nchi ya tatu barani Afrika kwa kupata kiasi kikubwa cha fedha kutokana na usimamizi mzuri wa Miradi inayofadhiliwa na GEF.

Dkt. Muyungi ameishukuru GEF kwa ushirikiano wake wa muda mrefu na Tanzania, huku akisisitiza umuhimu wa kuongeza upatikanaji wa rasilimali za kifedha kutokana na utajiri mkubwa wa Tanzania wa mifumo ikolojia ya nchi kavu, maji baridi na bahari, kuwa 32% ya eneo lote la ardhi imehifadhiwa.

Aidha, pande mbili zimejadili maandalizi ya GEF-9 National Dialogue, itakayowakutanisha wadau kujadili vipaumbele vya Tanzania chini ya GEF-9, kujifunza kutokana na utekelezaji wa miradi ya GEF-8 na kuweka vipaumbele vya miradi mipya yenye manufaa ya kimazingira, kijamii na kiuchumi. Miradi hiyo inatarajiwa kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, National Environmental Master Plan, NDC 3.0 na Mikakati mingine ya kitaifa.

Katika hatua nyingine, Tanzania imejitolea kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kikanda wa GEF unaotarajiwa kufanyika kati ya Septemba na Oktoba, 2026.

Habari

Settings