Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Ofisi ya Makamu wa Rais yapewa kongole kumuenzi Karume

Apr, 06 2026

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Hamza Hassan Juma ameipongeza Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwa kufanya Kumbukizi kifo cha Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

Mhe. Hamza ametoa pongezi hizo wakati akifunga Kongamano la kumbukizi ya miaka 54 ya kifo cha Hayati Sheikh Abeid Amani Karume katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, Aprili 6, 2026.

Amesema imezoeleka kuona kumbukizi ya kiongozi huyo ikifanyika mara nyingi Visiwani Zanzibar lakini kwa uamuzi ambao umefanywa na Ofisi ya Makamu wa Rais tena kwa kushirikisha wanafunzi kutoka vyuo vya elimu ya juu itawasaidia zaidi, kufahamu na kuelewa kuhusu waasisi wa Muungano.

Ameongeza kwa kusema elimu inayotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais kuhusu Muungano ni jambo kubwa kwa vijana ambao wengi wao bado hawajui misingi na chimbuko la Taifa la Tanzania.

“Kimsingi Hayati Sheikh Abeid Amani Karume na Mwalimu Julius Nyerere ndio waasisi wa Muungano wetu na viongozi hawa walikuja kuhitimisha tu kile ambacho Watanzania wenyewe tayari walikuwa wamekianzisha.

“Kabla ya Muungano wa Kiserikali, tayari kulikuwa na Muungano wa wananchi wenyewe na hata viongozi wetu kabla ya Muungano walikua wakikutana na kutembeleana,” amesema Mhe. Hamza.

Habari

Settings