Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais aagiza sera ya biashara bunifu kufungua fursa za kiuchumi kwa vijana

Oct, 19 2026

Makamu wa Rais, Mhe. Deogratius Ndejembi, ametoa miezi sita kwa Wizara ya Viwanda na Biashara kuandaa Sera mahususi ya biashara bunifu (startups), itakayosaidia vijana na wafanyabiashara kupata mitaji na hivyo kuongeza na kupanua wigo wa ubunifu na biashara nchini ikiwa ni mkakati wa kuchochea ajira na kujenga uchumi unaotegemea maarifa na teknolojia kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Akifungua Wiki ya Biashara Bunifu (Startups Week) leo, Oktoba 19, 2026, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam, Ndejembi amesema Serikali inatambua mchango wa biashara bunifu katika kukuza uchumi na kuzalisha ajira, hivyo imejipanga kuweka mazingira yatakayowezesha mawazo ya vijana kukua na kuwa biashara kubwa zenye uwezo wa kuvutia uwekezaji na kushindana katika masoko ya ndani na nje.

Amesema sera hiyo itazingatia mahitaji ya kipekee ya biashara bunifu, ambazo zina uwezo wa kukua kwa kasi na kuvutia uwekezaji mkubwa, tofauti na biashara ndogo na za kati (SMEs), huku akisisitiza umuhimu wa taasisi za fedha kuweka mifumo ya upatikanaji wa mitaji badala ya kutegemea mikopo pekee.

Katika hatua hiyo, ameitaja Benki ya NMB kuwa miongoni mwa taasisi zilizoanza kuwezesha biashara bunifu, huku akieleza kuwa Serikali itaendelea kufungua fursa za masoko kupitia utaratibu wa kutenga asilimia 30 ya manunuzi ya umma kwa makundi maalumu na fedha za uwezeshaji zinazofikia Sh bilioni 200, ambazo vijana wenye biashara bunifu wanaweza kunufaika nazo.

Katika kuondoa changamoto za mazingira ya kufanyia kazi, Makamu wa Rais ameielekeza Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu kuanzisha kituo cha pamoja cha ubunifu (innovation centre), itakayowezesha vijana kukutana, kubadilishana mawazo na kuunganishwa na wawekezaji wakubwa wa ndani na nje zikiwemo Taasisi za fedha. Amesema ushirikiano na benki, kampuni za mawasiliano na wadau wengine unaweza kuwezesha upatikanaji wa maeneo ya kazi na huduma muhimu, ikiwemo intaneti ya bure, huku akisisitiza Chama cha Biashara Bunifu Tanzania kushirikishwa kikamilifu katika maandalizi ya sera hiyo.

Aidha, Ndejembi amesema Tanzania ina fursa kubwa ya kukuza biashara bunifu kutokana na matumizi yanayoongezeka ya teknolojia na ukubwa wa soko la ndani na Afrika, akitaja takribani usajili milioni 120 wa simu nchini na watumiaji hai milioni 60, ambao asilimia kubwa wanatumia simu janja. Amewataja vijana Alvin na Ramadhan waliofanikiwa kuanzisha biashara bunifu na sasa ni Kampuni zenye mitaji mikubwa kama mifano ya uwezo wa Watanzania kutumia ubunifu kutengeneza fursa za kiuchumi, akisisitiza kuwa mazingira bora ya sera, mitaji na masoko yatawezesha biashara bunifu kuongeza mchango wake katika ajira na ukuaji wa uchumi kuelekea mwaka 2050.

Akichangia mjadala katika ufunguzi wa wiki hiyo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, amesema Wizara hiyo si polisi wala mgambo wa kufunga biashara, bali jukumu lake ni kuhamasisha, kulea na kukuza biashara pamoja na mawazo bunifu ya Watanzania. Amesema kwa kushirikiana na sekta nyingine, Wizara itaendelea kuhakikisha hakuna biashara inayofungwa bila sababu za msingi za kisheria, isipokuwa zile zinazokiuka au kuendeshwa kinyume na sheria za nchi, akisisitiza kuwa dhamira ya Serikali ni kujenga mazingira yanayochochea ukuaji wa biashara badala ya kuzikwamisha.

Kapinga amesema Wizara itaendelea kuhamasisha wananchi, hususan vijana, kubadili mitazamo na mienendo katika kufanya biashara, huku ikiimarisha ushirikiano na sekta binafsi kuhakikisha sera na sheria zinaendana na mabadiliko ya teknolojia na mahitaji ya biashara bunifu. Ameahidi kuwa kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Wizara itaendelea kuboresha mazingira ya biashara, kutangaza bidhaa na ubunifu wa Watanzania nje ya nchi na kuwezesha biashara bunifu kupenya katika masoko ya ndani na kimataifa.

Akitoa salamu za Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Albert Chalamila, amesema Dar es Salaam ni miongoni mwa wanufaika na wadau wakubwa wa biashara bunifu nchini, hivyo Mkoa utaendelea kuunga mkono jitihada za kukuza sekta hiyo kama sehemu ya kupanua fursa za kiuchumi na kuongeza ajira kwa vijana. Amesema Mkoa utaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuimarisha mazingira yanayochochea ubunifu na ukuaji wa biashara, ili kuwawezesha vijana kutumia maarifa na vipaji vyao kujiajiri, kuzalisha ajira na kuchangia maendeleo ya uchumi wa Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Biashara Bunifu Tanzania (Tanzania Startup Association), Bw. Paul Makanza, amesema chama hicho kilichoanzishwa mwaka 2020 kimeendelea kuwa kiungo muhimu katika kukuza biashara bunifu kupitia ushawishi, utafiti na ushiriki katika uandaaji wa sera zinazolenga kuboresha mazingira ya biashara nchini, hususan kwa vijana. Amesema chama hicho kimefanikiwa kuandaa ripoti ya mfumo wa biashara bunifu nchini (Startup Ecosystem Report), inayobainisha fursa na changamoto za sekta hiyo pamoja na namna inavyoweza kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Makanza amesema juhudi za chama hicho na wadau wake zimechangia kuzalishwa kwa takribani ajira 20,000 kupitia biashara bunifu, hatua inayoonyesha uwezo wa sekta hiyo kuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi na ajira kwa vijana. Hata hivyo, amesema changamoto ya upatikanaji wa mitaji na masoko bado inakwamisha ukuaji wa biashara nyingi bunifu, hivyo kusisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi na wadau wa ubunifu ili kuwezesha biashara hizo kukua na kuongeza mchango wake katika uchumi wa Taifa.

Kabla ya kushiriki mjadala kuhusu biashara bunifu, Makamu wa Rais alitembelea mabanda ya maonesho ya wabunifu na wawekezaji, wakiwemo wadhamini wakuu wa tukio hilo, Benki ya NMB, ambayo hadi sasa imefanikiwa kufadhili biashara bunifu sita zilizoingia katika mfumo wa benki hiyo, huku nyingine tano zikiwa katika hatua za mwisho za uwezeshaji. Hata hivyo, changamoto ya upatikanaji wa dhamana kwa mikopo mikubwa imeendelea kuwa kikwazo kwa biashara bunifu zinazohitaji mitaji zaidi ili kupanua shughuli zake na kuongeza mchango wake katika uchumi wa Taifa. ‎

Habari

Settings