Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Mradi wa hifadhi ya mazingira kunufaisha wananchi 6,000

Nov, 07 2026

Wananchi takriban 6,000 wanatarajiwa kunufaika moja kwa moja na miradi ya hifadhi ya mazingira yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 2 sawa na shilingi bilioni 5.2 kupitia ushirikiano wa Ofisi ya Makamu wa Rais na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Kiasi hicho cha fedha kimetengwa kusaidia mashirika 49 ya kiraia na mashirika ya kijamii yanayotekeleza miradi ya mazingira inayoongozwa na jamii Tanzania Bara na Zanzibar.

Hayo yamejiri wakati wa hafla ya makusaini makubaliano ya utoaji wa ruzuku hizo kati UNDP na Serikali ya Tanzania kupitia Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi.

Akizungumza katika hafla hiyo Dkt. Muyungi alisema Programu ya Ruzuku Ndogo (SGP) ni mpango endelevu unaokidhi mahitaji na vipaumbele vya jamii za wenyeji na kutaja mashirika 49 yaliyochaguliwa kuimarisha ushiriki wa jamii kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali ili kufikia matokeo endelevu na ya muda mrefu.

Kupitia Awamu ya 8 ya Uendeshaji ya Programu ya Ruzuku Ndogo ya Mfuko wa Mazingira Duniani (GEF), ruzuku hizo zitasaidia mipango katika maeneo matatu ya kipaumbele: Mfumo Ikolojia wa Serengeti, Tanzania ya Kati (Dodoma) na Zanzibar (Unguja na Pemba).

Maeneo hayo yatatoa maeneo muhimu ya kuzingatia kwa uhifadhi wa mazingira unaoongozwa na jamii, huku miradi ikishughulikia uhifadhi wa bioanuwai, urejeshaji wa mfumo ikolojia, kilimo endelevu, usimamizi wa pwani na baharini na maisha endelevu.

Asilimia 30 ya rasilimali za programu zitasaidia miradi nje ya mandhari hizi za kipaumbele, kuhakikisha kwamba jamii zaidi kote Tanzania zina fursa za kunufaika.

Habari

Settings