Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Kwagilwa: Mabadiliko ya tabianchi yanahitaji ushirikiano kuyakabili

May, 26 2026

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira Mhe. Reuben Nhamanilo Kwagilwa amesema mabadiliko ya tabianchi si suala la kesho bali ni changamoto ya sasa inayohitaji ushirikiano wa taasisi za elimu.

Amesema hayo wakati akizindua Kituo cha Jamii cha Ustahimilivu wa Mabadiliko ya Tabianchi (CCRC) kilichopo jijini Arusha Mei 26, 2026 jijini Arusha kitakachosaidia kuimarisha uwezo wa jamii kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi nchini.

Aidha, Mhe. Kwagilwa alisema kuwa alitoa wito kwa taasisi za umma na wadau kutoka Taasisi binafsi kuitia maagizo ya serikali kwa kushiriki shughuli za upandaji miti.

Aliongeza kuwa kwa kuanzishwa kwaa kituo hicho muhimu kitatakuwa daraja la maarifa, tafiti na suluhisho za changamoto za mazingira zinazoikabili jamii.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha TICD Dkt. Bakari George aliahidi kuwa kituo hicho kufanya tafiti, kujenga uwezo wa jamii pamoja na kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika shughuli za uhifadhi wa mazingira na matumizi endelevu ya rasilimali asilia.

Nae, Na Amon Anastaz Mpanju, Naibu Katibu Mkuu - Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, amemhakikishia mgeni rasmi kuhusu dhamira ya Wizara kuhakikisha TICD kuendelea kuwa kinara katika kuandaa wataalamu na jamii yenye uwezo wa kukabiliana na changamoto za maendeleo na mazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Habari

Settings