Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Katibu Mkuu aridhishwa ukaratabati jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais

Jan, 28 2026

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi ameeleza kuridhishwa kwake na ukarabati wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililopo Luthuli Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya ziara yake ya kukagua jengo hilo, Dkt. Muyungi ameipongeza kamati ya usimamizi wa ukarabati wa jengo hilo kwa kumsimamia vyema mkandarasi kukamilisha kazi hiyo inakamilika katika wakati na muda uliopangwa.

“Niwapongeza kamati ya ukarabati wa jengo hili kwa kazi kubwa na nzuri mliyoifanya, jambo muhimu ni kuhakikisha marekebisho madogo madogo niliyoyaona yanafanyiwa kazi ili tuweze kukabidhiwa jengo hili” amesema Dkt. Muyungi.

Aidha Dkt. Muyungi ambaye katika ziara hiyo aliongozana na Mwenyekiti wa Kamati ya ukarabati wa jengo hilo, Bw. Paul Laizer amesifu mfumo wa miundombinu ya TEHAMA iliyofungwa katika jengo hilo ambayo itarahisisha utendaji kazi kwa viongozi na watumishi.

Ameeleza kuwa katika ziara hiyo pia amejionea maboresho makubwa yaliyofanywa na kutoa maelekezo kwa mkandarasi kuhakikisha anafanyia kazi maoni na ushauri alitoa ili kuhakikisha jengo hilo linakamilika kwa wakati ili kuweza kutumika.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kamati ya usimamizi wa ukarabati wa jengo hilo, Bw. Paul Laizer amemhakikishia Dkt. Muyungi kuwa kamati yake ushauri, maoni na mapendekezo yanafanyiwa kazi ili kuwezesha kukamilika kwa jengo hilo.

Habari

Settings