Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Kamati ya Usimamizi Mardi wa SLR yakutana

Mar, 01 2026

Kamati ya Ushauri wa Kitaifa ya Usimamizi wa Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bioanuai (SLR) chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais, imekutana kwa lengo la kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Februari 27, 2026.

Kikao kazi hicho kimeongozwa na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Baraka Luvanda, pamoja na kukutanisha wajumbe wa kamati, wataalamu wa mazingira, wawakilishi wa taasisi za serikali, wadau wa maendeleo pamoja na washirika wa mradi huo ambao ni Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) kupitia Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na Shirika la Kimataifa la uhifadhi wa Mazingira (IUCN).

Aidha taarifa ya kina kuhusu maendeleo ya utekelezaji iliwasilishwa, ikionyesha mafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizojitokeza pamoja na mikakati ya kuimarisha utekelezaji wa mradi huo ambao upo ukingoni kuisha.

Akiwasilisha taarifa hiyo Mratibu wa Kitaifa wa Mradi Dkt. Damas Mapunda, amesema Mradi umefanikiwa kuendelea na shughuli za urejeshwaji wa maeneo yaliyoharibiwa, pamoja na kuhamasisha jamii kushiriki katika uhifadhi wa rasilimali asilia, na kuimarisha mifumo ya usimamizi wa mazingira, bioanuai, katika ngazi za mitaa na halmashauri.

Wajumbe wa Kamati walisisitiza umuhimu wa Kuongeza juhudi za upandaji miti na urejeshwaji wa maeneo oevu na misitu, Kuimarisha elimu ya mazingira kwa jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi, Kuweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, Kuimarisha ushirikiano baina ya serikali na jamii.

Pamoja na hayo, Kamati ilitoa maelekezo ya kuboresha maeneo yaliyo onekana kuwa na changamoto ili kuhakikisha malengo ya mradi yanafikiwa kwa ufanisi na kwa lengo kuu la kuunga juhudi za serikali katika uhifadhi wa mazingira na kutekeleza Dira 2050.

Kikao kazi hicho ni sehemu ya utaratibu wa ufuatiliaji na tathmini unaolenga kuhakikisha miradi ya mazingira inatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya kitaifa na kimataifa pamoja na kutimiza lengo zima la uhifadhi wa mazingira.

Habari

Settings