Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango, leo tarehe 17 Oktoba 2025 amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mazishi ya Kitaifa ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya, marehemu Raila Amolo Odinga.
Mazishi ya Kitaifa ya marehemu Raila Odinga yamefanyika katika Uwanja wa Nyayo Jijini Nairobi na kuhudhuriwa na viongozi kutoka mataifa mbalimbali pamoja na wananchi wa Jamhuri ya Kenya.
Makamu wa Rais aliambatana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo.
Marehemu Raila Odinga, alifariki tarehe 15 Oktoba 2025 na anatarajiwa kuzikwa tarehe 19 Oktoba 2025.