Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Dkt. Dugange: Uchumi wa Buluu uchukue nafasi vikao vya Muungano

Feb, 16 2026

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Festo Dugange ametoa rai kwa watendaji kulipa umuhimu suala la Uchumi wa Buluu katika vikao vya pande mbili za Muungano.

Amesema hayo wakati wa kikao cha ushirikiano kati ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kilichoketi Zanzibar leo Februari 16, 2026.

Dkt. Dugange amesema kuwa Zanzibar imepiga hatua katika eneo la uchumi hivyo kuendeleza ushirikiano Wake na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutaimarisha uchumi wa Taifa.

Alisema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais tayari imeanzisha Kitengo cha Usimamizi wa Uchumi wa Buluu ambacho ni fursa adhimu kwa wananchi kupata uelewa kuhusu sekta hiyo kupitia elimu inayotolewa.

Aidha, Naibu Waziri alisema kuwa ni muhimu kuzungumzia fursa za Muungano ikiwemo miradi inayotekelezwa katika pande zote mbili badala ya changamoto hivyo kuendelea kujenga imani kwa wananchi.

Pamoja na mambo mengine, aliongeza kuwa Muungano umekuwa ni chachu ya uchumi kwakuwa umeimarisha mazingira kupitia miradi ya maendeleo ikiwemo biashara ya kaboni ambayo inafanyika katika maeneo mbalimbali yakiwemo misitu na hata bahari.

“Tuwapongeze viongozi wetu wa kitaifa yaani Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuimarisha huduma za kijamii na miundombinu, yote hii ni katika kuwanuia wananchi w apande zote mbili za Muungano,” alisema.

Kwa upande Wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Mhe.Hamza Hassan Juma alishauri elimu ya Muungano iendelee kutolewa hususan kwa kundi la vijana.

Alishauri kuwatumia wasanii mbalimbali nchini katika kutoa elimu ya Muungano, kwani wengi wao ni vijana hatua itakayoisaidia kufikisha ujumbe kwa haraka zaidi.

Halikadhalika, Mhe. Hamza alitoa rai kwa watendaji kutoka Ofisi hizo mbili kutangaza zaidi fursa zinazopatikana katika Muungano badala ya changamoto akisema kuwa Serikali zote zinazishughulikia ili kuzimaliza.

Alipongeza juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kusimamia sekta ya uchumi ambao umeendelea kuimarika siku hadi siku kwa maendeleo endelevu.

Habari

Settings