Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Tanzania yapiga hatua matibabu ya saratani

Sep, 15 2026

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amesema Tanzania imepiga hatua katika mapambano dhidi ya saratani, kufuatia uwekezaji wa Serikali katika kinga, uchunguzi na matibabu, huku ikilenga kuongeza huduma hizo na kujijenga kuwa kitovu cha utaalamu na mafunzo ya tiba ya saratani kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Makamu wa Rais, amesema hayo wakati akihutubia Jukwaa la Kisayansi la Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomu (IAEA Scientific Forum) kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, linalofanyika Vienna nchini Austria.

Amesema chini ya uongozi wenye maono na dhamira thabiti ya kisiasa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, sekta ya afya imeendelea kuwa kipaumbele cha kitaifa, jambo linalodhihirishwa na maendeleo yaliyopatikana katika nyanja za kinga, utambuzi na matibabu ya saratani kuanzia ngazi ya msingi hadi ngazi ya juu ya huduma za afya.

Makamu wa Rais, ametaja hatua mbalimbali za mafanikio zilizofikiwa na Tanzania, kama kuongezeka kwa utoaji wa chanjo ya dozi moja dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi (HPV) kwa wasichana wenye umri wa miaka tisa hadi 14, kutoka asilimia 58 mwaka 2018 hadi asilimia 98 mwaka 2026, kuongezeka kwa vituo vinavyotoa tiba ya saratani kwa mionzi (radiotherapy) kutoka vitatu mwaka 2020 hadi sita mwaka 2026, hatua iliyoongeza upatikanaji wa huduma hiyo kutoka asilimia 14 hadi asilimia 26 na kunufaisha wagonjwa wapatao 6,500.

Amesema Serikali imelenga kufikisha vituo tisa vya huduma jumuishi za saratani katika kanda sita za kimkakati Tanzania Bara na Zanzibar ifikapo mwaka 2030, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kusogeza huduma za kibingwa karibu zaidi na wananchi. Hatua hiyo inaenda sambamba na uwekezaji mkubwa katika teknolojia za kisasa za uchunguzi na matibabu.

Aidha, Makamu wa Rais amesema, Tanzania imeanza kutumia mashine ya PET-Scan inayounganishwa na cyclotron, kifaa maalumu kinachowezesha uzalishaji wa isotopu za mionzi zinazotumika katika uchunguzi wa kisasa, na kuwa miongoni mwa nchi 10 za kwanza barani Afrika kutoa huduma hiyo.

“Kati ya mwaka 2021 na 2026, idadi ya mashine za MRI imeongezeka kutoka saba hadi 28, LINAC kutoka mbili hadi nane, CT Scan kutoka 12 hadi 97, mammography kutoka nne hadi 20, huku mashine za x-ray za kidigitali zikiongezeka kutoka 147 hadi 770”, alisisitiza Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais ametoa wito kwa Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomu (IAEA), Nchi Wanachama na washirika wa kimataifa kuendelea kuunga mkono uimarishaji wa huduma jumuishi za saratani nchini Tanzania, ikiwemo kufadhili miradi ya kitabibu iliyoainishwa katika mpango maalumu ulioandaliwa na Tanzania kwa kushirikiana na IAEA kupitia kauli mbiu ya Rays of Hope (Mionzi ya Matumaini).

Utekelezaji wa miradi hiyo unatarajiwa kuongeza huduma za uchunguzi, utambuzi na matibabu katika maeneo mbalimbali nchini na hivyo kupunguza idadi ya wagonjwa wanaolazimika kusafiri umbali mrefu au kufika katika hospitali, saratani ikiwa katika hatua za mwisho.

Katika hatua inayolenga kuipa Tanzania nafasi kubwa zaidi kikanda, Makamu wa Rais ametoa wito kwa Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomu (IAEA) kuiteua Taasisi ya Saratani Ocean Road kuwa Kituo cha Umahiri cha Saratani, ili kusaidia mafunzo na kujenga uwezo wa wataalamu kutoka nchi nyingine, hususan zile za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Jukwaa hilo limefunguliwa na Mkurugenzi Mkuu wa IAEA, Rafael Mariano Grossi, huku likiweka msisitizo katika kuendeleza mpango wa Rays of Hope, ambao Tanzania tayari inanufaika nao katika kujenga uwezo wa huduma za saratani.

Tanzania imetumia mkutano huo kueleza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano na IAEA katika matumizi mengine ya teknolojia ya nyuklia, ikiwemo kilimo na maandalizi ya muda mrefu ya programu ya nishati ya nyuklia.

Kwa Tanzania, mkutano huo unatoa fursa ya kuunganisha hatua ambazo tayari zimepigwa na mahitaji ya awamu inayofuata ya kuongeza vituo vya saratani, kujenga wataalamu, kupata teknolojia zaidi na kuimarisha ushirikiano wa kisayansi na kifedha.

Jukwaa hilo la siku mbili linafanyika chini ya kaulimbiu “Rays of Hope: Delivering on the Promise of Cancer Care,” likiwakutanisha viongozi, wanasayansi, wataalamu wa afya na wadau wengine kujadili namna ya kupunguza pengo la upatikanaji wa huduma za uchunguzi na matibabu ya saratani duniani.

Habari

Settings