Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

Kwagilwa atoa siku 3 kutatua tatizo la majitaka Arusha

Sep, 15 2026

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa ameuelekeza uongozi wa Mkoa wa Arusha ndani ya siku tatu kuitisha kikao cha pamoja kitakachohusisha Ofisi ya Mkoa, Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini) TARURA, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA), Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa lengo la kutafuta suluhisho la tatizo la maji taka yanayopita kwenye mifereji katika daraja lililopo karibu na Kiwanda cha A to Z.

Kwagilwa ametoa maelekezo hayo kwa niaba ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira) baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa hifadhi ya mazingira katika Kiwanda cha A to Z, ambacho kimewahi kudaiwa kutiririsha maji taka katika maeneo ya wananchi wakati wa mvua.

Baada ya kupata maelezo kutoka kwa uongozi wa kiwanda hicho, Serikali imeelezwa kuwa kiwanda kimekuwa kikitibu maji hayo na kimeshindwa kuyaruhusu kutoka nje kutokana na kukosa ushirikiano na taasisi husika kati ya taasisi hizo ili kupata njia sahihi ya kutiririsha maji hayo na sasa kimeomba ushirikiano wa Serikali katika kutatua changamoto ya mfumo wa maji taka unaopita kutoka katika kiwanda hicho.

Akitoa maelekezo hayo baada ya ukaguzi, Mhe. Kwagilwa amesema kikao hicho kitaitishwa na mkoa kinapaswa kuchambua hali halisi ya eneo hilo na kuweka mpango wa pamoja wa kudhibiti tatizo, huku akitaka kuhakikisha maji yanayotibiwa na kiwanda hayaendelei kuleta changamoto kwa mazingira na wananchi wanaozunguka eneo hilo.

“Kikao kikae ndani ya siku tatu na nipate taarifa na ndani ya siku saba nataka kupata taarifa kwa niaba ya Mhe. Waziri nipate taarifa ya nini mango uliopo mahali hapa, na nimepata taarifa kuwa mwendelezo wa mtaro huu pamoja na maji ambayo kiwanda kimejitahidi kuyatibu kitaalamu kabisa.” amesema Mhe. Kwagilwa.

Amesisitiza kuwa taasisi zote zinazohusika zinapaswa kushirikiana ili kupata suluhisho la kudumu, hasa katika kipindi hiki ambacho mamlaka inayohusika na utabiri wa hali ya hewa imetangaza uwepo wa mvua za El Niño.

Kwagilwa amemtaka uongozi wa Mkoa wa Arusha kuhakikisha kikao kinafanyika ndani ya siku tatu na taarifa ya hatua zilizochukuliwa kuwasilishwa kwake ndani ya siku saba.

Habari

Settings