Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Makamu wa Rais

'Changamoto za mabadiliko ya tabianchi ni fursa'

Sep, 15 2026

Serikali imesisitiza umuhimu wa kugeuza changamoto za mabadiliko ya tabianchi kuwa fursa za uwekezaji, ajira, ubunifu na ukuaji wa uchumi wa kijani nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa kufungua Mkutano wa Tanzania Green Summit 2026 katika Kituo cha Mikutano cha Mlimani City, Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, amesema mabadiliko ya tabianchi hayapaswi kutazamwa kama changamoto ya kimazingira pekee, bali pia kama eneo lenye fursa kubwa za maendeleo ya kiuchumi.

Waziri Masauni amesema kaulimbiu ya mkutano huo, “Turning Climate Action into Opportunity”, inaendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na mipango mbalimbali ya Serikali ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

“Tanzania ina fursa kubwa katika nishati jadidifu, nishati safi ya kupikia, kilimo endelevu, usimamizi wa taka, uchumi wa mzunguko, utalii endelevu, uchumi wa buluu na suluhisho zinazotegemea mifumo ya asili.”

Aidha, Waziri Masauni amesisitiza umuhimu wa kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kijani kupitia upatikanaji wa ujuzi, teknolojia, mitaji na masoko, akieleza kuwa vijana wanapaswa kutambuliwa kama wabunifu, wajasiriamali, watafiti na viongozi wa uchumi wa kijani, na si wanufaika pekee wa programu za tabianchi.

“Tanzania imechukua hatua mbalimbali katika agenda ya mazingira na tabianchi, ikiwemo kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa Kituo cha Afrika cha Vijana cha Mafunzo ya Mabadiliko ya Tabianchi, pamoja na Ofisi ya Kikanda ya Santiago Network on Loss and Damage, hatua zinazolenga kuongeza uwezo wa nchi zinazoendelea kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.”

Awali, Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Richard Muyungi alisema Tanzania inaendelea kutumia fursa zinazotokana na mifuko ya kimataifa ya mazingira na tabianchi, huku akitaja pia uwepo wa miradi ya biashara ya kaboni inayoratibiwa kupitia Kiutuo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni (NCMC).

Ameeleza kuwa fursa hizo zinapaswa kuendelezwa kwa kuzingatia utunzaji wa mazingira, uongezaji thamani ndani ya nchi, uhamishaji wa teknolojia na uundaji wa ajira kwa Watanzania.

Ushiriki wa vijana katika ajenda ya mazingira na tabianchi umepewa msisitizo maalum, huku wadau wakihimizwa kutowaona vijana kama wanufaika wa programu za tabianchi pekee.

Taasisi za fedha na wawekezaji pia wamehimizwa kuchukua nafasi kubwa zaidi katika mageuzi kuelekea uchumi wa kijani kwa kubuni mifumo bunifu ya fedha kwa ajili ya biashara za kijani na miradi inayostahimili mabadiliko ya tabianchi.

Wawekezaji wametakiwa kutouona uendelevu wa mazingira kama suala la kutimiza matakwa ya Sheria pekee, bali kama fursa ya kujenga thamani ya kiuchumi ya muda mrefu.

Habari

Settings