Waziri Jafo awataka wakandarasi kuzingatia matakwa ya sheria ya mazingira

Jul, 12 2021

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Selemani Jafo ametoa maelekezo kwa wakandarasi wenye miradi ya kuchimba mabwawa nchini lazima wafuatilie matakwa ya kimazingira ili kulinda afya za wananchi.

Jafo ametoa maelekezo hayo leo Julai 12, 2021 wakati wa ziara ya kukagua mabwawa ya kutibu majitaka katika mradi wa Reli ya Kisasa ya Standard Gauge katika eneo hilo.

Alionesha kutokuridhishwa na mradi huo huku akishangazwa na hatua ya kutokufuata masharti ya kimazingira kutoka Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira (DUWASA) na Jiji la Dodoma.

Aidha, Waziri Jafo ameipa wiki mbili Kampuni ya Yapi Merkez iwe imefukia mashimo iliyoyachimba kwa ajili ya kutengeneza mabwawa katika eneo hilo kutokana na la Zuzu kutokana na kutowashirikisha Duwasa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Alisema kuwa huu mradi ni wa kwetu wote lakini masharti lazima yafuateww ili kuepuka kuleta madhara kwa wananchi hasa uchafuzi wa mazingira.

Pia amewataka kujenga miradi ambayo itabaki na wananchi wataitumia hata baada ya kukamilka kwa miradi yao.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa NEMC Kanda ya Kati, Bw. Emmanuel Mwasilu alisema kabla ya Waziri Jafo kufika walifika katika mradi huo na kuonesha kutokuridhishwa na mazingira jinsi yalivyo.

Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo wamewachukua hatua ya kuipiga faini kampuni hiyo ya shilingi milioni 50 ikiwa ni pamoja na kuwaelekeza miundombinu iondoshwe mahali hapo na shughuli isitishwe.

Alisema Baraza hilo limeishasitisha lakini pia wanapaswa kufanya uchapushaji kuwa katika hali nzuri maelekezo mengine ya Waziri tunayachua kwa ajili ya kuwaelekeza wakandarasi wengine.Nitoe wito kwa wananchi Taasisi mbalimbali na Wakandarasi waweze kufuata sheria na maelekezo ambayo tunakuwa tumewapa katika vibali,”amesema.

Mtaalamu wa Mazingira kutoka kampuni hiyo, Aminiel Mlugarana aliahidi kuwa watayafunga mabwawa hayo na watashirikiana na DUWASA na NEMC kutafuta eneo jingine kwa ajili ya kufanya shughuli kama hiyo.

Naye Meneja DUWASA, Mhandisi Kashilimu Mayunga alisema maelekezo ambayo ameyatoa Waziri watayafuata na watashirikiana kuwapa utaalamu wa namna gani ya kuweza kujenga mabwawa hata kama ni ya muda mfupi.

Settings