Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

VICE PRESIDENT'S OFFICE

News

​Waziri Jafo awataka wafanyakazi kujiepusha vitendo vya rushwa


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo amewataka watumishi wa Ofisi yake kujiepusha na vitendo vya rushwa huku akionya kuwa yeyote atakayebainika kuhusika na vitendo hivyo hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yake.

Jafo aliyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Makamu wa Rais uliofanyika jijini Dodoma Aprili 23, 2021.

Akizungumza na Wajumbe wa baraza hilo, Jafo amewataka watumishi hao kuzingatia uadilifu na uwajibikaji katika utekelezaji wa shughuli za serikali na kuacha alama ya kudumu yenye ufanisi katika maeneo yao.

" Ndugu zangu tufanye kazi kwa juhudi na maarifa, kazi zetu ziwe za mfano kila mmoja ajivunie kuacha Legacy katika maeneo yetu, tuzingatie uadilifu katika kusimamia masuala ya Mazingira hususan suala la Mabadiliko ya Tabianchi na Masuala ya Muungano” Jafo alisisitiza.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mohammed Abdallah Khamis amewataka wafanyakazi wa Ofisi yake kuwa na vitu vinayopimika katika utekelezaji wa majukumu yao.

Khamis ambaye pia ni Naibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais aliendelea kusisitiza uwajibika katika kazi kwa wafanyakazi hao hatua ambayo itasaidia kuongeza tija katiia kuwatumikia wananchi.

Aliwataka wafanyakazi katika Ofisi hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano, kujituma na kuchapa kazi bidii bila kusukumwa kwa kuzingatia muda ili waweze kutimiza majukumu yao kwa wakati.

“Kila kiongozi katika Idara au Kitengo chake anawajibika kuwasimamia watumishi walio chini yake na mwenye kupata stahiki yake apate hivyo niwaombe tuwe na ushirikiano ili tuweze kuleta tija katika majukumu yetu,” alisisitiza.